BAADA YA chatu mkubwa kutokeza katika nyumba ya mfanyabishara mkubwa wa jiji la Arusha mengi yaibuka
akielezea tukio halisi mmoja wa mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye jina lake alijafahamika alidai kuwa yeye na mfanya kazi walikuwa wanakunywa chai sebuleni ndipo wakasikia kitu kinagonga katika moja ya chumba ambacho walishapigwa marufuku kukifungua
aliasema kuwa wakati kinaendelea kugonga ndipo walipoamua kwenda kufungu chumba hicho wakiwa na mfanya kazi ili waone nini kinachogonga
mara tu baada ya kufungua chumba kile walisema walikutana uso kwa uso na chatu huyo ndipo walipoamua kukimbia na kupiga kelele
kutokana na shutuma hizi za kudaiwa chatu huyu alikuwa anafugwa na mfanyabiashara huyo aliyetambulika kwa jina la joseph magessa timu nzima ya libeneke la kaskazini ilijitaidi kutafuta ukweli huu kwa kumtafuta mwenye nyumba magesa au mke wake ili aelezee tukio hili lakini hazikufanikiwa kwani tulivyofika nyumbani akuwepo na tulivyojaribu kupiga simu yake haikupatikana hatukuishia apo bali tulimtafuta pia mke wake lakini atukumpata.
taswira halisi ya eneo la tukio imeonekana watu wengi kutoka katika sehemu mbalimbali wakienda kushuhudia kama tukio hilo ni lakweni na wengine walienda kuangalia mabaki ya nyoka uyo aina ya chatu