Mbunge wa Jimbo la
Hai, Freeman Mbowe akishuhudia uharibifu kwenye moja ya madarasa ya
Shule ya Msingi Weruweru iliyoko wilayani Hai, ikiwa ni sehemu ya ziara
yake anayofanya pamoja na kamati yake ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo
(CDF), kwa ajili ya kutathmini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
jimboni kwake ili mfuko huo uweze kusaidia kuongeza nguvu za ujenzi.
Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko huo alielezwa kuwa shimo
hilo limekuwa likitumika na wananchi waovu kama 'mlango' wa kuingia na
kutoka kwa ajili ya kuiba kuni zinazotunzwa katika chumba hicho cha
darasa.
Mmoja
wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF) Jimbo la Hai
akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Shirimatunda
iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe
(Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza nguvu za
ujenzi. Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya
kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha
wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya
vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.