Baadhi ya watoto wa shule za msingi jijini Dar
wakifanya mazoezi ya maigizo kwa ajili ya tamasha la kesho kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa.
Na
Mwandishi wetu
WANAFUNZI wa shule za Msingi nchini, wameshauriwa kuwa na
mazoea ya kusoma vitabu kwa lengo la kuwa wagunduzi wa vitu
mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Soma, Demere Kitunga wakati wa maandalizi ya tamasha la kwanza
la vitabu vya hadithi kwa watoto wa Shule za msingi.
Kitunga amesema kuwa tamasha hilo ni moja ya michakato ya
kuwataka watoto kupenda kusoma vitabu hasa vitabu vya hadithi kwa nia ya
kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii.
"Ugunduzi wa jambo fulani unaanzia katika kusoma hivyo
watoto wakiwa wanania ya kusoma vitabu mbalimbali hususani vya hadithi
wataweza kuongeza uwelewa fulani katika fikra zao,"amesema
Kitunga
Aidha
amesema kuwa tamasha hilo linatarajia kuanza kesho hadi juni 14 mwaka huu
katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini ,ambapo Mgeni rasmi
anatarajia kuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mmoja wa watoto akionyesha kipaji chake wakati wa
mazoezi kwa vitendo kupitia hadithi mbalimbali walizosoma kutoka kwenye
vitabu.
Kitunga amesema kuwa Taasisi hiyo hadi sasa imeweza
kusambaza vitabu katika Shule mbalimbali za Msingi pamoja na klabu za
kujisomea zikiwemo Kurasini ,maktaba pamoja na
Chang'ombe.
Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na maigizo ambayo
yatafanywa kwa kutumia hadithi zilizokuwa katika vitabu hii yote kwa lengo
la kukuza utamaduni wa watoto kusoma vitabu.