|
Askofu
Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua
Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko
wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii. |
|
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake
Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao
na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru. |
|
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa amekumbatiana na
Mchumba wake Bi Anande Nnko muda mfupi baada ya kumtafuta kwa muda
katika sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwa Bi Harusi Mtarajiwa
,Meru. |
|
Bi
,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe
Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika
nyumbani kwao Meru. |
|
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimvisha pete ,Mchumba
wake Anande Nnko akati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao
na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru. |
MBUNGE
wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia
kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga
lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani
ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya
Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa
Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba
mchana watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi
jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.
"Nichukue
tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana
wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la
kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds
kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.
Na
ssari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe
hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo
mbalimbali