Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. Joseph Komwihangiro, Mkurugenzi wa Marie Stopes kwa kuwa mstari wa mbele
katika huduma na elimu za mzazi wa mpango Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma za uchunguzi wa
saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika
uwanja wa Chipukizi mkoani humo. Wengine toka kushoto ni Mama Salma
Kikwete, Mlezi wa MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa, Mwenyekiti wa MEWATA, Mhe.
Kebwe Steven Kebwe (Mb.), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kulia kabisa
ni Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Ismail Aden Ragge.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea Jumamosi
Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa
kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi
mkoani humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na wanakwaya wa kambi ya Msange JKT ya Tabora Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua huduma za uchunguzi wa
saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika
uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete ameamuru Jeshi la Polisi kupeleleza na kisha kuwachukulia hatua mara
moja watu wote wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika
mkoani Tabora.
Rais Kikwete amesikitishwa sana na tuhuma hizo
zilizosababisha kuwepo kwa tatizo la muda mrefu kwa wakulima
wa tumbaku kwa kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika kwa muda mrefu.
Alisema: "Kwa upande wa tatizo la wakulima wa
tumbaku kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika nimeelezwa na
kulielewa. Kuna tuhuma za wizi na ubadhilifu.
“Nimemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi
atume watu wake wa upelelezi wa makosa ya Jinai waje wafanye uchunguzi ili
wahusika wakamatwe na kufikishwa Mahakamani na kupewa adhabu
zinazostahili.
“Ameniahidi kuwa keshokutwa (Jumatatu)
watu hao watakuja. Wapeni ushirikiano unaostahili ili
tukomeshe uhalifu na dhuluma zinazofanywa na Maofisa wa Vyama vya Ushirika na
taasisi za fedha kwa muda mrefu sasa".
Rais aliyasema hayo Jumamosi Mei 7, 2014
wakati akizindua huduma za uchunguzi wa
saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika
uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais Kikwete alisisitiza
kwamba zoezi la kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa wizi na ubadhilifu katika vyama
vya ushirika lisifanywe la kisiasa, na kwamba asiogopwe wala kuonewa haya mtu
yeyote anayehusika hata awe nani.