eketaji.
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla
ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa
Ukeketaji Nchini Tanzania. Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji
Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es
Salaam.
Washiriki
Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini wakiwa
katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,
Sophia Simba Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.
SERIKALI imesema
kitendo cha baadhi ya makabila kuendeleza mila za kuwakeketa wanawake
na watoto ni ukatili mkubwa ambao umekuwa na madhara kiafya kwa
anayetendewa. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba alipokuwa akifungua
Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji nchini Tanzania
unaofanyika kwa siku mbili katika Mkumbi wa Mikutano wa Kunduchi
Hoteli.
Waziri
Simba alisema ukeketaji ni udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike
na umekuwa ukihatarisha maisha ya wahusika kwa matokeo ya vifo, vilema
na maradhi kama vile fistula na magonjwa mengine hivyo kutaka kila mmoja
kuungana kuupinga. Alisema kwa upande wa Serikali imekuwa ikishirikiana
na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inatokomeza mila hizo pamoja na
ukatili mwingine wa kijinsia.
“Wengi
hapa ni mashaidi wa madhara ya ukeketeji ikiwemo vifo, vilema na
maradhi kama vile, fistula na mengineyo. Serikali inalaani na kukemea
ukatili huu unaomdhalilisha mwanamke na kumletea madhara makubwa,”
alisema Waziri Simba. Aidha alisema ili kupambana na hali Serikali
imesaini mikataba mbalimbali ya kukabiliana na ubaguzi anuai hasa kwa
wanawake na pia kuanzisha Dawati la Jinsia kila sekta kukabiliana na
vitendo vya kikatili nchini. “…Serikali iliandaa na inatekeleza mpango
wa taifa wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto
(2001-2015) na mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji (2001-2015)…,”
alisisitiza Waziri Simba.
Aliongeza
pamoja na hayo na juhudi mbalimbali za Serikali ukatili huo kwa
wanawake na watoto hauwezi kuzuiliwa kwa sheria na mipango ya serikali
hivyo kuitaka jamii pamoja na wadau wengine kuunganisha nguvu kupambana
na vitendo hivyo hapa nchini. “….Suala la kutokomeza ukatili wa
kijinsia, halitakwisha kwa kutegemea Serikali au sheria peke yake. Ni
jukumu letu wadau wote kwa pamoja kukemea na kupiga vita kwa nguvu zote,
kutoa elimu dhidi ya ukatili, huduma kwa wahanga na kuhakikisha
wanaotenda na kubariki vitendo hivi wanachukuliwa hatua,” alisema.
Akizungumza
katika mkutano huo, Naibu Mwakilishi wa UNFPA Tanzania, Mariam Khan
alisema licha ya juhudi zinazofanywa kupambana na ukeketaji nchini, kila
mwaka vipindi vya ukeketaji bado wasichana na watoto wanaokeketwa
wamekuwa wakipoteza maisha bila sababu ya msingi kutokana na madhara ya
ukeketaji jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa. Aliwataka washiriki kwa
pamoja kujadiliana nini cha kufanya ili kukomesha ukatili huo
unaoendelea kushamiri nchini na kuahidi kuwa UNFPA itaendelea kuunga
mkono juhudi za mapambano hayo kwa kutoa mafunzo na kuwezesha shughuli
za mapambano hayo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia