MKATABA WA BILIONI 2.1 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA MAJI KATA ZA KIVULE NA KIPUNGUNI WASAINIWA NA MANISPAA YA ILALA

 Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa Akiwasili kata ya Kipunguni na kupokelewa na Diwani wa kata Hiyo Na Viongozi wengine .
 Mkandarasi wa kampuni Kika Construction Mbaraka Kihawe akimkaribisha Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kwenye meza kuu.
 Mwanainchi Huyu alipatwa na Furaha sana Kumuona Mh Jery Silaa akashindwa kujizuia na kwenda Kumsalia.
 Wageni waliokuja kuhudhuria utiaji sahihi wa mikataba baina ya manispaa ya Ilala na Wakandarasi wakiwa meza kuu

Kaimu mkuu wa Idara ya Maji Bi Selestina John akiongelea jinsi mradi huo wa maji kwa kata mbili za Kivule na Kipunguni ni namna gani zitanufaika na mradi huo mara tu baaada ya kukamilika mwezi wa kumi na mbili.Ambapo kwa kata ya Kivule wataweza kupata maji lita laki nne na themanini(480000) kwa siku,wakati kata ya Kipunguni B wataweza kupata maji lita  laki mbili na themanini na tano elfu(285,000) kwa siku.



 Diwani wa Kata ya Kivule Mh Nyasika Getama Akishukuru manispaaa kwa kuweza kuikumbuka kata yake katika mradi huo mkubwa wa maji kwa kata Hizo mbili
Mwakilishi wa Diwani wa kata ya KipunguniB akishukuru pia kwa kuweza kupewa mradi wa maji kwenye kata yao ya kipunguni B

 Meya wa Manispaa ya Ilala Mh Jerry Silaa akielezea ni kwani wameamua kuja kutiliana sahihi mbele ya wanainchi ili kuweka uwazi na uwajibikaji wa kila mmoja,kuanzia Manispaaa mapaka kwa Wakandarasi.Hivyo amewataka  Wakandarasi hao kuwa makini na kufanya kazi kwa viwango ili kuweza kutatu Tatizo la Maji katika kata Hizo mbili.
 Mkandarasi wa kampuni ya
 Mkandarasi kutoka Kika Construction Mbaraka Kihawe wa pili kutoka kushoto akitia sahihi mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji kata za Kipunguni B na Kivule na Manispaa ya Ilala,Meya Wa Manispaa ya Ilala(mwenye miwani)akishuhudia Mwanasheria wa Manispaa Kulia akitia sahihi Mikataba Hiyo.
Mwanasheria wa Manispaa Mashauri Musini Kulia akitia sahihi Mikataba Hiyo Huku akishuhudiwa na Viongozi wa kata za Kipunguni B na Kivule.
 Mkandarasi wa Kampuni ya JP Traders  wa Pili kutoka Kushoto akitia sahihi mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji baina yake na Manispaa Ya Ilala,Kulia ni mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Mashauri akihakiki na kutia sahihi mikataba hiyo.
 Meya Wa manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa akikabidhiana Mikataba na Mkandarasi kwa Ajili ya mradi wa maji kwa kata za Kipunguni B na Kivule
Wanainchi wa kata Za Kivule na Kipunguni B wakifuatilia utiaji sahihi wa mikataba hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post