. Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Godfrey Zambi ameuagiza uongozi wa kiwanda cha CETAWICO kuhakikisha
unalipa deni la Sh700milioni unalodaiwa na wakulima wa zabibu ndani ya
mwezi huu wa sita kabla Serikali haijachukua hatua nyingine.
Zambi alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki
alipotembelea wakulima wa zabibu ambao walimweleza kilio chao kuhusu
deni la muda mrefu ambalo wanadai kiwanda hicho.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa zabibu,
katibu wa Ushirika wa Wakulima wa Zabibu na Masoko, Rashid Mkombozi
alisema wanamdai mwekezaji huyo kwa zaidi ya miezi 9, hali
inayowasababishia ugumu wa maisha kutokana na wengi wao kushindwa kulipa
mikopo.
Mkombozi alisema pamoja na jitihada mbalimbali
walizofanya zikiwemo kushirikisha serikali ya wilaya na mkoa ili
kusaidiwa kudai madeni yao, bado wamegonga mwamba kutokana na kutopewa
ushirikiano na badala yake kuishia kupewa majibu yasiyoridhisha.
Alisema siyo mara ya kwanza kwa mwekezaji huyo
kutolipa madai yao kwani hata mwaka jana msimu wa mwezi wa pili ilibidi
Waziri wa Kilimo, Chrisopher Chizza, aingilie kati ndiyo wakalipwa
kidogo. Hivyo waliomba aondolewe kutokana na kudharau wazawa ili aletwe
mwingine atakayeshirikina nao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia