Na
Mwandishi Wetu
Warembo 16
leo watawania taji la Miss Tabata 2014 kwenye shindano ambalo litafanyika
katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa
shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa mrembo atakayeshinda atamrithi Dorice
Mollel ambaye pia anashikilia taji la Miss Ilala.
Mratibu
huyo amesema mshindi huyo atazadiwa 500,000/- wakati mshindi wa pili atapata
300,000/- na watatu 200,000/-. Mshindi wa tatu na wa nne kila moja atapata
150,000/-.
Bali na
zawadi ya pesa taslim pia kila mshiriki atapata zawadi ya kujisomea kwa mwaka
moja katika chuo cha Data Training College. Thamani ya kila kozi kwa kila mmoja
litakuwa ni 800,000/-.
Warembo
waliyosalia watazawadiwa 100,000/- kila
mmoja.
Washiriki
ni Esther Frank Kiwambo (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22),
Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wengine ni
Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20), Ambasia Lucy Mally (22), Angle
Kashaga (22), Faudhia Hamisi Feka (21), Najma Charles Mareges (19), Lightness
Olomi (18), Husna Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) , Marry Henry (22) na Mariam
Shwaib Hussein (19).
Mratibu
huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya Twanga
Pepeta.
Miss
Tabata inadhaminiwa na Zanzi, Redds, Fredito Entertainment, CXC Africa, Saluti5
na Nevada Barber Shop.Miss
Tabata inaandaliawa na Bob Entertainment na Keen Arts.