Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/
kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji
wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada
ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show
mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze
safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia
GAIRO mjini.
Kwenye
gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine
wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa
mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa
Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza. Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.