Serikali
imetakiwa kutazama upya uwezekano wa kubadili sheria inayomnyima haki ya kuendelea na masomo
mwanafunzi wa kike pindi anapopata ujauzito akiwa shuleni.
Kauli hiyo
imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa elimu taaluma ,mkoa wa Arusha,Kabesi
katundu Kabeja wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa umoja wa wakuu wa
shule za msingi kutoka nchi ya Kenya uliofanyika katika hotel ya Leons iliyopo
Sakina kwa Idi ,jijini hapa,ambapo walimu zaidi ya 1000 kutoka nchini
humo walikutana.
Alisema hatua ya sasa ya kumfukuza shule mwanafunzi
wa kike mwenye ujauzito ni kumnyanyapaa na kumkosesha fursa ya kupata elimu,hivyo
alisema ni vema serikali katazama upya sheria hiyo kandamizi.
Aliitaka
serikali kuiga nchi jirani ya kenya ambayo sheria yao inaruhusu msichana
huyo kuendelea na masomo pindi anapokuwa
amejifungua.
‘’Hapa kwetu
sheria zinakataza mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo lakini
serikali tumeiomba serikali ibadili sheria hiyo ili kutoa fursa kwa mwanafunzi
mwenye ujauzito kuendelea na masomo pindi anapojifungua,alisema Kabeja.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa umoja kutoka nchini Kenya
,Wintred Mbinyasila ,alisema mkutano huo ambao umekuwa ukifanyika kila mwaka
unalenga kubadilishana mawazo na mwaka huu lengo ni kujifunza teknolojia ya
kufundishia.
Hata hivyo
alisema nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa suala la elimu kwa mtoto wa kike
baada ya kuruhusu mwanafunzi huyo pindi anapokuwa na ujauzito kuendelea na
masomo baada ya kujifungua.
‘’Serikali
huchukua hatua kali kwa mtu mzima aliyempa ujauzito mtoto wa kike ila kama
alipata ujauzito kutoka kwa mwanafunzi mwenzake ,sheria inaruhusu kuendelea na
masomo kwa masharti ya kutoa matunzo
pindi akifikia umri wa mtu mzima’’alisema
Naye mjumbe
wa shirikisho la walimu wakuu wa nchi za Afrika mashariki ,Anjelina Kitigwa
alisema mkutano huo unasaidia sana kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto
zilizopo hali itakayosaidia kuinua elimu
katika nchi za afrika mashariki.