Ticker

6/recent/ticker-posts

MBOWE KIONGOZI WA CHADEMA YOYOTE ATAKAE LETA UDINI KATIKA CHAMA TUNAMFUKUZA

chama demokrasia na maendeleo chadema kimesema hakiungi mkono swala laudini linaloendelea nchini na kuwataka watanzania wote kuishi kwa amani na upendo pasipo kuweka ukabaila wala udini na kutaka hatua za makusudi zichukuliwe na serikali juu ya swala hili.
akizungumza katika ufunguzi wa wam kutano wa baraza la CHADEMA kanda ya kaskazini mwenyekiti wa cha chadema mh FREEMAN MBOYE amesema chake chake hakiiungi swala la ugomvi wa kidini unaondelea nchini  na  kuwataka wanajamii kila mmoja kuamini katika dini yake na serikali ya ccm iweze kuchukua hatua maadhubuti dhidi ya swala hili.

Kisha mh mboye akatoa ufafanuzi kuhusu sera ya kuigawa tanzania katika majimbo anasema kila mtanzania anafursa ya kuishi popote,na watanzania wote wana uraia mmoja na paspot moja ya tanzanai,na mtazania anauhuru wa kugombea uongozi katika sehemu yoyote ya tanzania hivo kugawa majimbo si kama kugawa wantazia katika makabila na mpango wa kanda ni mpango unaokwenda kukijenga chama kutoka katika vyomba mpaka kwenye damu .
i wachadema kanda ya kaskazini pamoja na viongozi wake wa ngazi za juu ambapo hapo kesho watakwenda kufungua mkutano katika viwanja vya ngarenaro jijini arusha kwa ajili ya opersheni ya kuwatambua wanachama ya chadema kutoka nyumba kumi kumi.na kuwaanda kifkra na kupanga mikakati ya kuchukua nchi 2015na  sio opereshini bali ni kazi ya kudumu


Post a Comment

0 Comments