Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Lake
Tanganyika kuhitimisha sherehe za miaka 36 ya chama hicho mjini Kigoma
leo
Ngoma za utamaduni zamfurahisha Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Akipungia kwa furaha maelfu ya wananchi wa Kigoma wanaomshangilia kwa nguvu
Licha ya vyombo kukorofisha msanii Diamond nma kundi lake walitumbuiza kwa ustadi
Diamond akipagawisha
Mwenyekiti
wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa hotuba
yake kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Maadhimisho ya Miaka
36 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,
Mkoani Kigoma jioni hii.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisema machache,muda mfupi kabla
ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo
pichani} kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii.
Waziri
wa Uchukuzi,Dkt. Harisson Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa
Kigoma jioni hii na kuwahakikishia kuwa sasa hivi mkoa wa Kigoma mambo
yako vyema kabisa na treni itaendelea kufanyaka kazi kama zamani.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akiongoza shughuli hiyo.
Mwenyekiti
wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa
Kigoma,wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,kuongoza
Maadhimisho ya 36 ya kuzaliwa kwa CCM,Mkoani Kigoma leo.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia burudani ya ngoma.
Chipukizi
wa CCM Mkoa wa Kigoma wakifanya Gwaride la heshima kwa Mwenyekiti wa
CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka
36 ya kuzaliwa kwa CCM,yaliyofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika Mkoani Kigoma.
Mtangazaji mkongwe wa TBC Taifa Swedi Mwinyi akiwa hai hewani na wenzie
Katibu Mkuu wa CCM akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Omar Chambo na Maafisa waandamizi wa wakala wa usafiri wa anga
Washindi wa kombe la CCM 2013
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea banda la Uhuru na Mzalendo
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mang'ula akipitia magazeti ya zamani kwenye banda la Uhuru na Mzalendo
Ankal akiwa na wanahabari wa Kigoma
Ngoma toka mkoa wa Makamba nchini Burundi
Wanahabari waliorekodi sherehe hizo kutoka vyombo mbalimbali
Mablogger
wakirekebisha mitambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akihutubia. Kutoka shoto ni Ahmad, Othman, Bukuku, Nkoromo na
Mroki.