Bishop Thomas O. Laizer |
FAMILIA ya marehemu
Baba skofu Thomas Laizer wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania
dayosisi ya kaskazini kati imesema kuwa hayati Baba askofu ameacha wosia mzito
kwa waumini, wachungaji na viongozi wa kanisa hilo baada ya yeye kupita.
Akizungumza nyumbani kwa askofu huyo katika eneo la Nduruma
mke wa askofu huyo Mama Maria Laizer alisema kuwa mume wake kila mara alikuwa
anasisitiza kuwa kazi aliyoianzisha iendelezwe na isiharibiwe kwa vyovyote
vile.
“Baba askofu alisisitiza
jambo hili hata kwa wote waliofika kumjulia hali akiwa kitandani kwake kuwa
wahakikishe kuwa kazi aliyoianza inaendelezwa “alisema Mama Laizer.
Alileza kuwa alikuwa na mume wake masaa machache kabla ya
kifo chake na kwamba mchana wa siku aliyoaga dunia alikuwa na hali nzuri lakini
baadye hali yake ilibadilika na kuondokewa na uhai.
Alisema kuwa askofyu huyo alianza kusumbuliwa na maradhi ya
kansa kwa kipindi cha miaka minne iliyopita lakini hakuweza kupata tiba stahili
kwa haraka.
“Alikuwa akilalamika maumivu katika tumbo lake mara kwa mara
na baadaye alizidiwa tukampeleka Nairobi akatibiwa lakini baada ya muda alianza
tena kulalamika maumvu na ndipo akapelekwa India na kugundulika kuugua kansa
ambayo tayari ilikuwa imesambaa mwilini”alisema Mama Laizer.
Marehemu Baba askofu Thomas Laizer ameacha mjane watoto wanne
na mjukuu mmoja.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Askofu wa
kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania
dayosisi ya kaskazini kati Askofu Thomas lazier amefariki Dunia jioni ya
leo.
Habari ambazo
zimethibitishwa na katibu Mkuu wa dayosisi hiyo Israel Ole Karyongi zimesema
kuwa askofu alikumbwa na mauiti majira ya saa
12 za jioni ya leo.
“Ni kweli
baba Askofu amepita na tuko katika hali ya dharura ngumu na tungependa mtuachie
nafasi ili tuwape taarifa juu ya msiba huu kesho”alisema Karyongi akizungumza kwa
njia ya simu .
Askofu lazier
ndiye askofu wa kwanza wa na mwanzilishi
wa dayosisi hiyo ambayo awali ilikuwa
ikiitwa dayossi Mkoani Arusha kabla ya mwaka juzi kubalishw ajina na kuitwa dayosisi
ya kaskazini kati.
Ni msiba
mkubwa mno katika Mkoa wa Arusha kutokana na askofu huyo kupata umaarufu katika kazi zake za kiroho na
kijamii husasan jamii ya kabila la wamasai.
Anatajwa kushiriki
katika kuendeleza jamii hiyo kielimu kwa kubuni na kuanzisha shule zaidi ya
ishirini za sekondari zikiwemo maalum kwa ajili ya watoto wa kike.
kufuatia
msiba huo,Waziri Mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowasa amesema kuwa kanisa
na jamii limempoteza kiongozi na mpigania maendeleo ya jamii kiroho na
kimwili.
“Tumepoteza
kiongozi wa kiroho na kijamii,amehusika katika kuelimisha jamii kwa kuanzisha
shule nyingi za Sekondari,amehusika pia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Arusha
Lutheran Medical Center,zahanti na vituo vya afya katika vijiji kadhaa Mkoani Arusha pamoja na hoteli ya Corridor springs”alisema
Lowasa.
Aliwataka waumini wa kanisa la KKKT kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na kiongozi wao.
"Natoa
pole nyingi kwa familia ya marehemu Baba Askofu Laizer na kanisa la
KKKT kwa ujumla wake,lakini askofu Laizer atakumbukwa kwa utumishi
uliotukuka katika siku za uhai wake"alisema Lowasa akihojiwa na kituo
cha radio cha kitaifa cha Radio one asubuhi ya leo
Aidha aliwapongeza madaktari wa hospitali ya Seliani kwa jitihada zao za kumsaidia baba askofu akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
Aidha aliwapongeza madaktari wa hospitali ya Seliani kwa jitihada zao za kumsaidia baba askofu akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia