JUMUIYA ya
umoja wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) mkoani Arusha juzi walifanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa mbalimbali
katika hopsitali ya mko ya Mt,Meru ambapo katika ziara hiyo waligawa vitu
mbalimbali ikiwa ni njia mojawapo ya kuadhimisha miaka 36 ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM).
Katika ziara
hiyo umoja huo pia ulipata fursa ya kutembelea wodi ya wazazi katika hospitali
hiyo ambapo walipita kuwafariji sanjari na kuwakabidhi mahitaji mbalimbali kama
sabuni,khanga na mafuta ya kujipaka kwa ajili ya watoto wliozaliwa.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi bidhaa hizo mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha,Flora
Zelothe alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuadhimisha miaka 36 ya chama chao
ambao wameona njia sahihi ya kuadhimisha ni kuwatembelea wagonjwa hao.
Alisema kuwa
waliona njia pekee ya kuadhimisha shrehe hizo ni pamoja na kuwatembelea
wakinamama waliojifungua katika hospitali hiyo kwa kuwa kuzaaa si kazi rahisi.
“Tumeona
njia sahihi ya kuadhimisha sherehe hizi ni kuwatembelea wakinamama
waliojifungua amoja na wagonjwa hapa hospitalini kwa kuwa kuzaa si kazi rahisi
kama mnavyodhani”alisema Zelothe
Hatahivyo,alisisitzia
kuwa umoja wao umetoa khanga zenye picha ya marehemu Bibi Titi Mohamed kwa
wakinamama waliojifungua kama ishara ya kuuenzi mchango wake kwa kuwathamini wakinamama enzi za uhai wake.
Alisema kuwa
nembo ya umoja wao na picha ya mama na mtoto hivyo kwa kutoa khanga hizo
wameonyesha mchango wao katika kuthamini kundi la akinamama na watoto ndani ya
jamii bila kujali itikadi za vyama vyao.
Naye,mjumbe
wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Arusha,Violet Mfuko aliwapongeza wahudumu
mbalimbali ndani ya hospitali hiyo ya mkoa huku akiwataka wafanye kazi zao kwa
uhadilifu kuwajali wagonjwa wote bila ubaguzi.
Mfuko,kwa
kujiamini akitoa shukrani kwa uongozi wa hospitali hiyo aliwaambia wahudumu hao
kuwa wakumbuke kazi ya uuguzi ni ya kujitolea huku akiwapongeza kwa kuonyesha
moyo wa ukarimu kwa wagonjwa hao.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya wagonjwa waliokaidhiwa bidhaa hizo ndani ya wodi ya
wazazi,Hawa Kidio aliupongeza umoja huo pamoja na chama cha CCM huku akisema
wameonyesha mfano wa kujitolea bila ubaguzi ambao unapaswa kuigwa na vyama
vingine.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia