Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi
ya Kaskazini Kati, la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa
heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa
Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), kwenye Kanisa Kuu la KKKT jijini Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati
nyumbani kwa Askofu mara baada ya kutoa heshima zake za mwisho
kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT jijini Arusha,
Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Fredy Maro wa Ikulu