BREAKING NEWS

Tuesday, February 12, 2013

NGORONGORO ,SERENGETI NA MLIMAKILIMANJARO YAFANIKIWA KUINGIA KATIKA MAAJABU SABA YA VIVUTIO BARANI AFRIKA

??????????????????????TANZANIA kupitia shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) limefanikiwa kuingia katika maajabu saba katika bara la Afrika kupitia vivutio vyake vitatu bora vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na Hifradhi ya Serengeti ambavyo viliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi zingine hali ambayo itafanya Sekta ya utalii hapa nchini iweze kukua na kuimarika


Katika picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla hiyo.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David Kafulila.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.
Mama Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.
Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema  kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB)  Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi  katika hafla hiyo, kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.
  Akitangaza matokeo hayo jana mjini hapa, rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani,alisema kuwa katika kinyanganyiro hicho Tanzania imepata ushindi kwa kuwa vivutio vya aina yake.

Alitaja vivutio hivyo kuwa ni Pamoja na Mlima Kilimanjaro,hifadhi ya Serengeti pamoja na bonde la Ngorongoro ambapo vivutio hivyo viliweza kupigiwa kura nyingi sana na hivyo kuvipa ushindi wa hali ya juu huku  ndani ya vivutio hivyo kuna maajabu ya aina mbalimbali ambavyo havipatikani popote barani Afrika na duniani kwa ujumla

“leo nina furahi kutangaza kuwa Tanzania imeingia ndani ya maajabu saba na hivyo basi hii ni kama changamoto ya kuhakikisha kuwa bado mnaendelea kufanya viendelee kukua na kuinarika zaidi ili hata wakati mwingine muwe na vivutio vingi zaidi’aliongeza Dkt Imler.

Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema kuwa nchi za Afrika zina vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii huo.

Alisema anaamini kutokana na sifa ambayo Tanzania imeipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.

Aliongeza kuwa ndani ya Nchi  ya Tanzania kwa sasa wamejiwekea juhudi za makusudi kuanzia ngazi ya kitaifa ambapo kupitia ngazi mbalimbali wataweza kuharakisha maendeleo ya utalii hususani utalii ili maajabu mbalimbali ya Tanzania yaweze kufahamika duniani.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema ushindi huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la Watanzania wote kujivunia.

kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa hapa nchini(TANAPA)Alan Kijazi alisema kuwa wanatarajia mapato kuongezeka hasa katika mlima Kilimanjaro,bonde  la Ngorongoro, na hifadhi za Serengeti kwa kuwa vivutio hivyo vimetangazwa rasmi kama vivutio venye maajabu ya kutosha

Alisema Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na Watanzania waendelee kuutunza, Ngorongoro alisema kuwa imeshinda kwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven: simba, tembo, viboko, nyati, vifaru, sokwe na mamba.

Kijazi aliongeza kuwa pamoja na kutangazwa kwa vivutio hivyo lakini bado TANAPA limejiwekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanaendeleza shuguli za utalii hapa nchini ingawaje bado kuna changamoto kubwa sana kwenye masuala ya utalii wa ndani

??????????????????????
Rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani akitangaza matokeo hayo
??????????????????????
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo akihutubia mara baada ya kutangazwa kwa vivutio hivyo
??????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
????????????????????????????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????

??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates