TAARIFA
ILIYOIFIKIA libeneke la kaskazini HIVI PUNDE TOKA VISIWANI
ZANZIBAR,INATUHABARISHA KUWA PADRI EVERIST MUSHI (PICHANI) WA KANISA
KATOLIKI HUKO ZANZIBAR,AMEPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WASIOJULIKANA
NA KUFARIKI PAPO HAPO ASUBUHI HII WAKATI AKIELEKEA KWENYE IBADA KATIKA
KANISA LA MTONI,ZANZIBAR.
SABABU ZA KUPIGWA RISASI KWA PADRI HUYO BADO HAZIJAFAHAMIKA MPAKA SASA.
MASHUHUDA
WA TUKIO HILO WANASEMA KUWA WATU HAO WALIOFANYA TUKIO HILO WALIKUWA NI
WAWILI NA WALIKUWA WAMEPAKIZANA KWENYE PIKIPIKI AINA YA VESPA WAKATI
PADRI HUYO ALIKUWA KWENYE GARI LAKE AMBALO BAADA YA KUTOKEA KWA TUKIO
HILO NALO LILIACHA NJIA NA KWENDA KUGONGA NYUMBA MOJA ILIYOKUWA JIRANI
NA KANISA HILO.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO NA TAARIFA ZAIDI ZITAWAJIA KILA ZITAPOPATIKANA.