Ticker

6/recent/ticker-posts

KLABU MPYA YAZINDULIWA ARUSHA AFRIKA MASHARIKI NA KATI HAKUNA KAMA IYO USIPIME NI WORLD GARDEN

 Huu ni muonekano wa jengo la world garden inavyoonekana kwa nje
 apa ni geti kuu la kuingialia katika jengo la world garden ilipo mushono ndani ya jiji la Arusha
 katikati mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa mulongo akiwasili kuzindua rasmi jengo hili la world garden
 wadau mbalimbali walishiriki katika uzinduzi wa ukumbi huu wa world garden ambapo katika jengo hili kuna vitu mbalimbali ikiwemo ukumbi wa disco afrika mashariki na kati hakuna kama huu kwani ni mkubwa na pia ni mzuri kuliko yote
 mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo akizindua jiwe la msingi katika jengo hilo

 mkuu wa mkoa wa arusha kiwa na mkurugenzi mtendaji wakiwa wanakata utepe wa lango kuu la kuingialia katika jengo hilo
 mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya world garden wakiwa wanatembelea jengo hilo mbara baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi apa ni ngazi za kuingilia katika ukumbi wa disco

mkuu wa mkoa akiwa na vingozi wengine pamoja na wageni waalikwa wakiangalia jinsi jengo hilo lilivyo ndani hapa wapo ndani ya ukumbi wa disco







 mkuu wa mkoa akiteta jambo na mkurugenzi mtendaji wa world garden



 picha juu na chini maeneo mbalimbali ya ukumbi huo ikiwemo sehemu za kupumzikia ukiwa disco au klabu

 hii ni kaunta ilikuwa bado aijawekwa vinjwaji lakini ndo muonekano wake huo


 apa ndipo dj wanakaa kufanya mambo
huu ni ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya jengo hilo la world garden usipime na usiache kutembelea kwa kesho ambapo ni siku ya wapendanao kutakuwa na disco zuri kutaka kwa madj wakali ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 tu 

 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa wetu katika madhari  na hadhi ya jiji

Aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo jijini hapa lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata ya mshono ndani ya jiji la Arusha

Alisema kuwa   mkoa wa arusha kwa sasa umepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo ni wajibu wa wazawa kuwekeza katika mambo mbalimbali  akitolea mfano kuwa mpaka sasa pamoja ya kuwa   wananchi ni wengi na wageni ni wengi lakini mpaka sasa kuna sehemu super makerti moja tu kitu ambacho kinatia aibu kwa jiji kubwa kama hili

Alisema kuwa viwanja vipo vya kujengea sehemu hizo ni watu wa kuwekeza tu hivyo aliwasihi wawekezaji wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika vitu mbalimbali ili kuweza kuwezesha jiji letu kuwa la kimataifa

Alibainisha kuwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wanaogopa kwenda kuchukumikopo na kuwekeza katika vitu mbalimbali lakini aliwatoa hofu na kuwaambia kuwa mikopo ipo na ni haki ya kila mmoja kwenda kuchukuwa mkopo kwani nafasi zipo wazi na mikopo ipo ya kutosha huku akibainisha kuwa amna mfanyabishara yeyote mkubwa anafanya kitu pasipo kuchukuwa mkopo

Alipongeza uongozi wa kampuni ya world garden na kudai kuwa wameweza kupiga atua kubwa kwani kufungua kwao kwa jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kwani vijana wengi watapata ajira kupitia jengo hilo kwani katika jengo hilo kuna vitu vingi kwama vile ukumbi wa disco watu wa usafi wa nje na mengine mengi ambapo watu wote wanaotakiw akufanya kazi huku  ni watanzania vijana hivyo watakuwa wamesaidia vijana kupata ajira

 Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji wa World garden alisema kuwa wao kama kampuni yao inampango wa kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 120 na pia alisema kuwa watajitaidi kuboresha vitu mbalimbali .


Post a Comment

0 Comments