RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA LEO, PIA AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MALAGARASI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuzindua ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakifunua kitambaa cha jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
Rais Kikwete akiongezana na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier mara baada ya uzinduzi huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakipata maelezo juu ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma toka kwa mhandisi George Sambali wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi,Bw. Phillipe Dongier akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
Msanii Diamond na kundi lake wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo ya Daraja la Maragarasi kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa ujenzi wa Daraja hilo,Bw. Jung-Sik You kutoka nchini Korea,leo Januari 4,2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Mama Salma Kikwete na maafisa mbali mbali wakikagua ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi lililopewa jina la Daraja la Kikwete mkoani Kigoma leo Februari 4, 2013. Asilimia zaidi ya 90 ya ujenzi wa daraja hilo zimekamilika nan linatarajiwa kufunguliwa baadaye mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Muungano eneo la Kibaoni wilayani Uvinza, Kigoma, akiwa njiani kuelekea mjini Kigoma, akitokea kukagua ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi leo.Picha na IKULU.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post