MBOWE AITAKA SERIKALI NA CCM IJIBU MAPIGO YA MAUJI YA VIONGOZI WA DINI GEITA,NA ZANZIBAR

 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Freeman Mbowe akiwa anaongea na viongozi wa chama kutoka katika mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni arusha ,kilimanjaro ,manyara pamoja na tanga kuhusiana na sera ya majimbo leo jijini Arusha
 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman Mbowe akiwasili katika ukumbi wa bugaloo kwa ajili ya kuongea na viongozi wa vyama mbambali kwa jili ya kupanga mkakati wa chama chao
 mwenyekiti wa  muda wa  chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kanda ya kaskazini ambaye pia ni mbunge wa karatu akiwakaribisha viongozi mbalimbali wa kanda ya kaskazini katika kikao cha viongozi wa chama hicho kanda  kikao ambacho kinajadili seraya majimbo
 picha juu na chini wajumbe ambao ni viongozi walioudhuria mkutano huo



KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida mwenyekiti wa chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA),Freeman Mbowe amesema kuwa mauji ya Viongozi wa
dini ambayo yametokea,katika mkoa wa Geita, na Zanzibar ni matokeo ya
CCM,na hivyo kama wataandelea kuendesha nchi kwa msingi hiyo bado nchi
itakabiliwa na mauji makubwa sana

Mboye aliyasema hayo mapema leo wakati akizindua kanda ya kaskazini
kwa chama hicho ambayo itaweza kuhudumia mikoa ya kanda ya kaskazini
katika shuguli za kichama na za kijamii

Alisema kuwa hapo awali Chadema kilishasema kuwa CCM isipuuzie
matatizo ya ubaguaji wa dini lakini chama hicho hakikusikia na badala
yake kiliendelea kujiendesha kwa misingi ya kubaguana kidini hali
ambayo sasa inanyima watu uhuru wa kuabudu na kufanya mambo yao

Alisistiza kuwa kama CCM  bado iliendelea kufanya ubaguzo wa dini kwa
misingi kuwa inakomoa Chadema lakini hawakujua na kutambua kuwa hali
hiyo inafanya mauaji ya kila siku ambayo sasa yameanza Geita lakini
Leo yameelekea Zanzibar mara baada ya Padre kuuliwa wakati akielekea
Kanisani kusalisha misa

“Leo kila mahali unasikia mauji ya dini lakini mimi nilishawaambia CCM
kuwa hiii sio hali ya kuendelea kuangalia lakini walujua  kuwa ni
siasa na wao  walifanya hivi kwa malengo ya kuwa wanatukomoa sisi
Chadema kwa kugawa Taifa katika Imani ya kidini sasa wamelikoriga
wanatakiwa kulinywa’aliongeza Mbowe

Katika hatua Nyingine Mbowe alisema kuwa wao kama Chadema wanalaani
Mauji ambayo yanatokea kila siku ndani ya Tanzania na kwa hali hiyo
hawataweza kuwagawa wananchi  katika misingi ya kidini kwa kuwa wote
wapo sawa na kama Nchi itaendeshwa hivyo ni wazi kuwa damu ambazo
hazina hatia zitamwagika kila mara.

“Chadema tunaalani kwa kweli haya mauji na kwetu Muislamu, Mkristo
wote ni wa moja na kamwe kiongozi ambaye ataonesha ubaguzi dhidi ya
wakristo na waislamu ni wazi kuwa tutamkimbia hatuwezi kuingiza
jitiada za CCM ndani ya chama chetu,na kuweka utaratibu wa kumwaga
damu ambazo hazina hatia kabisa’aliongeza Mbowe

Akiongelea suala la kanda ya kaskazini ndani ya chama hicho alisema
kuwa hiyo ni moja ya mikakati ambayo imewekwa na mbali na hilo pia
kupitia viongozi wa kanda ya kaskazini wataweza kujiwekea nafasi nzuri
sana ya kuchukua Nchi ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2015 hivyo
kufanya Nchi iwe huru zaidi kuliko  ilivyo kwa sasa

Mbowe aliongeza kuwa kanda ya kaskazini pia itaweza kuwa chachu ya
Maendeleo kwa kuwa itaweza kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo
zinawakabili kwa kuwa sasa kazi za maendeleo zitafanywa chini ya mikoa
minnne tofauti na hapo awali ambapo kila mkoa ulikuwa unajitegemea kwa
shuguli za kichama na za kichama.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post