WAKINA MAMA 3000 WATESWA NA FESTULA KILA MWAKA
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
ZAIDI ya akinamama 3,000 nchini Tanzania huugua ugonjwa wa
fistula mara baada ya kujifungua kila mwaka, huku sababu kubwa ya kupatwa
na ugonjwa huo ikiwa ni huduma duni za afya ya uzazi hasa zile huduma za
dharura kwa wajawazito wanapokuwa wakijifungua.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk.
Natalia Kanem alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya
Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani.
Lakini robotatu ya wagonjwa hao hawana uelewa wa kwamba wanaweza kupata
matibabu na kupona kabisa ugonjwa huo.
Ipo haja ya kuongeza bajeti ya
huduma kwa wahusika na kutoa elimu zaidi ili kusaidia jamii hii
inayoangamia kila kukicha kwa matatizo ya fistula.
Wakinamama na wasichana
ambao hukumbwa na matatizo ya fistula wamekuwa wakipata changamoto kubwa
baada ya kutengwa na familia zao na wengine kuvunjika ndoa zao kutokana na
hali ya kuvuja mkojo muda wote huku wakitoka na harufu kali.
Alisema ili
kuunga mkono juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa fistula.
Hata hivyo ili kupambana na ugonjwa huo, Dk. Kanen alisema kuanzia mwaka
2003 UNFPA na wadau wenzake ilizinduwa kampeni ya dunia nzima kuhakikisha
inazuia ugonjwa wa fistula (Grobal Campaign to End Fistula) mradi ambao kwa
sasa unafanya kazi kwa zaidi ya mataifa 50 ulimwenguni huku ukijikita kwa
kuzuia, kutibu na kuwasaidia kiuchumi waathirika wa ugonjwa huo.
Hali hiyo imewafanya washindwe kujiendeleza katika shughuli zao za kila
siku za kujiongezea kipato, Takribani akinamama 800 wanakufa kila siku
dunia nzima kutokana na matatizo ya uzazi huku 20m kati yao wakijikuta
wameathiriwa vibaya na ugonjwa hatari wa fistula.
Inakadiliwa kuwa kati ya
akinamama 50,000 hadi 100,000 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula ni
20,000 tu ndio hufanikiwa kupata matibabu ya ugonjwa huo kwa mwaka.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda
Msangi akizungumza na wanahabari kuzungumzia maadhimisho hayo yanayoanza
tarehe 23 Mwezi Mai, 2015 alisema hospitali hiyo na washirika wake
inasapoti maeneo manne ya wagonjwa wa fistula ambayo awali yalionekana ni
changamoto kwao.
Aliyataja maeneo hayo ni pamoja na Matibabu kwa wagonjwa, Gharama za
Usafiri, Gharama za Chakula na Gharama za Malazi ili kumsaidia mgonjwa
kuweza kukabiliana na changamoto hizo.
"...Tunaomba kila mmoja kuanzia
ngazi za familia watoe elimu kwa wahusika waje hospitalini kupata matibabu
mapema kwani ugonjwa huu unatibika," alisema Naibu Mkurugenzi wa Hospitali
ya CCBRT, Brenda Msangi.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia