SERIKALI imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na kujenga
mazingira mazuri ili kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika, ikiwa ni
pamoja na kuwavutia wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza katika
tasnia ya filamu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa Tuzo za
Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela
Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za filamu.
Dk. Mukangala alipongeza juhudi za baadhi ya wafanyabiashara wa filamu na
wasambazaji ya kudhibiti uharamia wa kazi za filamu, lakini aliwataka
kuifanya kazi hiyo kwa manufaa ya wadau wote na sio kwa manufaa binafsi.
"...Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanya biashara ya
filamu yanaimarishwa. Pamoja na hayo ni vyema wasambazaji na wafanya
biashara wengine wa filamu wenye uwezo wakaepuka kulidhibiti soko la filamu
kwa nanufaa yao binafsi ili kujenga ushindani sawa," alisema Dk.
Mukangala.
Aliwataka wasanii na wadau wote wa filamu kuhakikisha wanaboresha kazi zao
zaidi na kufuata vigezo vinavyotambulika ili kuzitangaza kazi zao hata nje
ya nchi. "Napenda mtambue kuwa ubora wa bidhaa za filamu ni moja ya vigezo
vya kuwa na soko bora la filamu, kwani filamu bora hujitangaza zenyewe.
Tuhakikishe kuwa tunaongeza weledi na ubunifu.
Hivi ndivyo vigezo
vilivyoifanya sekta ya filamu nchi zilizoendelea kufika hapo ilipo,"
aslisema Waziri Dk. Mukangala.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA), Simon
Mwakifwamba aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga chuo maalumu
kwa ajili ya filamu ili kuijengea uwezo zaidi tasnia kwani inamchango
mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa makundi anuai.
Waliojishindia tuzo za filamu kwa mwaka huu 'Tanzania Film Awards 2015
(TAFA)' katika vipengele mbalimbali ni pamoja na Irine Sanga (Best Screen
Play), Hissan Muya (Best Actor Supporting Role), Grace Mapunda Best Actress
Supporting Role), Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian), Irene Paul
(Best Actress), John Kalage (Best Director) na wengineo.a
Tuzo za filamu nchini 'Tanzania Film Awards' 2015 (TAFA).
Tuzo hizi kubwa
ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere International Conference Center. Zimewezeshwa na Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International Eye
Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani
Production.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia