Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha wakiwa
kwenye mkutano ambao walitoa tamko la kupinga uongozi wa chama wilaya
kuwaburuza kwenye mchakato wa ubunge wilayani humo.
Arusha.Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Monduli zaidi ya 600 wamewatuhumu
viongozi wa chama hicho kwa kuwaburuza katika maamuzi na kuwaamulia
nani atakua mbunge wa Jimbo hilo baada ya Mbunge wa sasa,Edward Lowassa
kutajwa kutogombea nafasi hiyo.
Wana CCM
hao kutoka Kata zote 20 walidai kumekuwepo na ukiukwaji wa makusudi wa
kanuni za chama unaongozwa na Katibu wa CCM wilaya,Elisante Kimaro
kufanya ziara za kichama na mmoja wa waliotajwa kugombea ubunge jimbo
hilo na kumtambulisha kinyume na kanuni za chama hatua iliyozusha
mgogoro na kuhatarisha uhai wa chama.
Katika
barua yao kwa Katibu wa CCM mkoa,Alphonce Kinamhala inawataja moja kwa
moja Mjumbe wa kamati ya Siasa ya mkoa,Paulo Kiteleki ambaye ni Katibu
Tarafa ya Kisongo,Mjumbe wa Kamati ya Siasa na maadili wa wilaya
,Kalaine Lowassa,Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake(UWT)wilaya,Einoti
Leringa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli,Edward
Sapunyu.
Wengine wanaotuhumiwa kukiweka
chama rehani kwa maslahi yao ni Mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya
ambaye pia ni diwani wa Kata ya Monduli Juu,Bariki Sumuni na Katibu wa
Hamasa wa Umoja wa vijana(UvCCM)Kimani Ndiarakombe.
“Tunaomba
viongozi wetu wakumbuke ya kuwa kuwepo CCM ni kuwepo kwa wanachama
ambao haki zao zinaheshimiwa na kupewa demokrasia ndani ya chama chao na
sio viongozi wa ngazi husika wanaamuakwa maslahi yao kukiuka taratibu
za chama kwasababu wamepewa dhamana ya kuwa viongozi.”ilisema sehemu ya
barua hiyo
Hata hivyo Katibu wa CCM wilaya
ya Arusha ,Elisante Kimaro alikanusha taarifa hizo na kudai hazina
msingi wowote bali kinachofanyika ni ziara ya kawaida ya kuwashukuru
wananchi kutokana na ushindi mkubwa walioupata kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka jana ambapo Mbunge wa Viti Maalum,Namelok
Sokoine ni Mjumbe ambaye ametoa mchango mkubwa kwa wanawake na vijana.
Mwakilishi
wa Kata ya Lorkisale,Lembrisi Klamian na Parmelo Ngoyo kutoka Kata ya
Sepeko walisema zama za kuburuzwa zimepitwa kila jambo linapaswa
kufanyika kwa ushirikishwaji na sio kuwapandikiza wagombea wao bila
ridhaa za wanachama.
Wanachama hao wamesema
iwapo malalamiko yao hayatashughulikiwa ipasavyo na kwa wakati
kwasababu wanaolalamikiwa ni wajumbe wa kamati za maamuzi ngazi ya
wilaya na mkoa watalazimika kutafuta njia mbadala ya kufikisha
malalamiko yao kwa uongozi wa ngazi ya taifa.
Wanachama
Teshi Oloing’ola kutoka Kata ya Lepurko na Osidai Nadongala wa Kata ya
Mbwakiri walisema kinachowasikitisha ni kuwa wajumbe wa kamati ya siasa
na kamati ya maadili wilaya kwenye kampeni za kumnadi mgombea
anayenadiwa na msimamia taratibu za chama ambaye ni Katibu wa wilaya.
Hata hivyo walidai viongozi hao wa wilaya kutumiwa na mmoja wa viongozi wakubwa wilayani humo bila kutaja jin