Meza kuu. (Picha zote na Geofrey
Adroph
Mshehereshaji wa Semina Bi. Rose
Mwalongo akiwakaribisha washiriki wote waliofika kwenye semina ya siku
mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International
Association of women in radio and television (AWRTT) kwa kushirikiana na
Ethical Journalism Network ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali
kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika.
Bi. Rose Haji Mwalimu kutoka
IAWRT Tanzania akifungua semina kwa kwa washiriki ambao walikuwa ni
wanahabari (hawapo pichani) mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na
nchi za Afrika wa pili kutoka kushoto ni Rais wa IAWRT Bi. Rachael
Nakitare, wa pili kutoka kulia ni Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen pamoja na
Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN).
Rais wa IAWRT Bi. Rachael
Nakitare akitoa semina kwa wanahabari namna ya kusimama katika ukweli na
uwazi na pia kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii, na
baadae kusababisha machafuko kwenye Uchaguzi mkuu wa
2015.
Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen
kutoka ubalozi wa Norway akiwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa makini
kipindi chote wanapochukua au kutafuta taarifa ili kuondoa vurugu kwa nchi
hasa Tanzania inayotegemea kufanya uchaguzi mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ethical Journalism
Network (EJN), Aidan White akitoa semina kwa wanahabari pamoja na wadau wa
habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi mazuri ya uandishi hasa kwenye hiki
kipindi cha Uchaguzi.
Baadhi ya washiriki wa
semina.
Rais wa Shirikisho la waandishi
wa Habari Afrika (FAJ), Mohamed Garba.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na
Uwajibikaji wa LHRC, Bi. Imelda Lulu Urio akielezea kuhusu vyombo vya
habari vya Tanzania vilivyoanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo
hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia
maana zinaleta chuki kwa taifa hasa suala la udini ambalo limeonekana
kushika kasi hapa chini Tanzania.
Bi. Irene Burungi Mugisha kutoka
IAWRT nchini Uganda akizungumza jambo.
Wadau wakifuatilia mada kwa
umakini.
Mhariri mkuu wa gazeti la The New
Times la nchini Rwanda, Bw. Kennedy Ndahiro akitoa mada kwa wanahabari
pamoja na wadau wa habari waliohudhuria kwenye semina ya matumizi mazuri ya
vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka
huu.
Rais wa Umoja wa waandishi nchini
Uganda, Bi. Lucy Ekadu akiwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika
utoaji wa habari katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotegemea
kufanyika mwaka huu na pia kutoa elimu ya msingi kwa wanahabari ili
kutochochea vurugu.
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha
Dar es Salaam, Dk. Ayoub Rioba akitoa semina kwa washiriki (hawapo pichani)
akiwasilisha mada yake kwenye semina iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock
jijini Dar.
Mshiriki Borry Mbaraka akiuliza
swali kwa watoa mada.
Rais wa IAWRT, Bi. Rachael
Nakitare (wa tatu kutoka kushoto) akiuliza swali kwa mtoa mada (hayupo
pichani).
Mtafiti wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe akiwasilisha mada yake kwa
wanahabari(hawapo pichani).
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa mmoja wa watoa mada wakati
wa semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Peacock jijini
Dar.
Mweka hazina kutoka IAWRT
Tanzania, Razia Mwawanga akikazia jambo kwenye semina ya
wanahabari.
Wadau wakifuatilia kwa umakini
mada.
Washiriki wa Semina hiyo wakiwa
katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu Ikiwa Tanzania inajiandaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, waandishi wa habari nchini wameaswa kujiepusha na lugha za chuki pamoja na uchochezi kipindi chote cha uchaguzi jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko kama inavyoonekana katika nchi mbalimbali barani Africa na duniani. Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network (EJN) ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika mashariki kwa lengo la kujadili masuala yanayohusiana na lugha za chuki kwa vyombo vya habari vya Afrika pamoja na madhara yake kwa wananchi. Akifungua warsha hiyo mgeni rasmi ambaye ni Raisi wa shirikisho la wanahabari Africa (FAJ) Bw. Mohamed Gabra amesema kuwa moja ya mambo ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko makubwa katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla ni lugha zinazotumika na wanahabari wakati wakiripori baadhi ya habari lugha ambazo amesema kuwa zimekuwa zikileta chuki baina ya watu na mwisho wake kusababisha madhara makubwa ambayo yangeweza kuepukika kama hatua zingechukuliwa mapema. Ametolea mifano kwa nchi kama Rwanda, Kenya, na nchi nyingine za ulaya ambazo zimewahi kuingia katika machafuko ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi kutokana na vyombo vya habari pamoja na wanahabari wenyewe kutumia kalamu zao kuwajengea chuki wananchi na mwisho kusababisha kuibuka kwa machafuko makubwa. Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya uchaguzi mkuu kwa mafanikio na amani ni lazima wanahabari wahakikishe kuwa wanasimama kwenye ukweli na kuhakikisha kuwa wanawaambia wananchi kile ambacho kinatokea na sio kujenga na kutengezeza maneno ambayo mwisho yatasababisha chuki kwa watanzania. Awali akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Rais wa (IAWRT) Bi. Rachael Nakitare amesema kuwa ni lazima kipindi hiki cha Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu ni kipindi cha wanahabari kusimama katika ukweli,uwazi na kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii,na baadae kusababisha machafuko. Baadhi ya watu waliotoa mada katika warsha hiyo ni pamoja na wakili na Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi. Imelda Lulu Urio ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea jinsi vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia mambo hayo ili kuepuka mambo makubwa ambayo yanaweza kujitokeza hapo baadae. Wengine waliopata nafasi ya kuchangia katika warsha hiyo ni mwandishi mkongwe nchini ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk. Ayoub Rioba ambapo amesema kuwa katika chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika kwa sasa wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wanahabari kutaka kujinufaisha wao kisiasa bila kujali madhara ambayo yanaweze kutokea endapo wanahabari watakiuka maadili ya taaluma zao. Baadhi ya wanahabari kutoka mataifa ya nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda,wamesema kuwa hakuna tofauti kubwa sana kati ya ufanyaji wa kazi za wanahabari zinazofanywa nchini Tanzania na mataifa yao bali tofauti iliyopo ni sheria zinazowaongoza wanahari katika mataifa hayo.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia