Taasisi
isiyo ya kiserikali ya Gola iliyoko
jijini Arusha imeanzisha Jukwaa la Kiongozi tunayemtaka linalotoa elimu ya
uraia kwa itakayowasaidia wananchi
kupata viongozi bora watakaosukuma gurudumu la maendeleo ya nchi.
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo Elisha Maghembe amesema kuwa tayari wameanza kuyakutanisha
makundi mbalimbali ikiwemo Wananchi na Vyama
vya siasa na kufanya midahalo mbali mbali ambayo inawajengea uwezo wananchi
kujua kiongozi gani anayefaa kuwaongoza.
“Tunapoelekea
uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu elimu ya uraia ni muhimu tunawaambia wananchi
wasikubali kulubuniwa na kuchagua viongozi wabovu watakaoligharimu taifa letu”
Alisema Maghembe
Elisha alisema
kuwa wamefanya midahalo katika baadhi ya kata zilizoko jiji la Arusha ikiwemo
Kaloleni,Sekei,Kijenge, Ungalimited huko wamehamasisha wananchi kujitokeza kwa
wingi kutimiza haki yao ya msingi kwa kujiandikisha na kupiga kura kumchagua
kiongozi wanayemtaka.
Alisema kuwa
miongoni mwa vyama vya siasa ambavyo wamekutana navyo na kufanya midahalo na
majadiliano ni pamoja na CHADEMA ,CCM na CUF bado wanaendelea na juhudi za
kukutana na vyama vingine.
“Kumekua na
sintofahamu ,Vyama vinawaweka wagombea ambao wananchi hawawataki ,midahalo hii
inasaidia vyama vya siasa kukutana na haja za wananchi na pia kufanya kampeni
kwa amani na utulivu pindi wanapoanza mchakato wa uchaguzi” Alisema Elisha
Jukwaa hilo
linatarajia kuwasaidia wananchi kuwapata viongozi makini ,viongozi bora kuanzia
ngazi ya chini ya madiwani,wabunge mpaka Raisi.