Uandikishaji Wanachama 'Tanzania Bloggers Network' (TBN),
Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers
Network' - TBN kilichosajiliwa rasmi na Serikali Aprili 2015 na kupewa
namba ya usajili; S. A 20008 kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na
chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na
waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na
Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa
kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu
ianze kuendeshwa mfululizo ambayo ipo hai. Kwa wakazi wa Dar es Salaam
wenye sifa na wanataka kujiunga na TBN fomu zinapatikana kwenye Ofisi za
Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market
lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama
muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni
Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi
mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN
kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa
shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa
siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la
utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media Group, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa wanachama wa mikoani juu na namna ya kujiunga wasiliana nasi kwa barua pepe; mushijoa@gmail.com au piga namba; 0756469470.
Kwa wanaoitaji kujiunga mnaombwa kuchukua fomu mapema kabla ya zoezi la usaji lililoanza 22 Aprili, 2015 halijafungwa.
NB;-
Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini
coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Hata hivyo utaratibu unafanywa wa
kuichapa kwenye soft coppy katiba hiyo na itatumwa mikoani kwa gharama
za TBN.
Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia