Tuzo za Watu 2015 zinatarajiwa
kufanyika Ijumaa ya May 22 kwenye hoteli ya Hyatt Regency (The Kilimanjaro)
jijini Dar es Salaam. Tuzo za mwaka huu
zinahusisha vipengele 13 vilivyopo kwenye muziki, filamu, redio, televisheni na
blogs.
Washindi watapatikana kwa asilimia
100 ya kura za wananchi zinazoendelea katika hatua hii ambapo wamebaki
washiriki watatu katika kila kipengele.
Kila mshindi atapokea tuzo na zawadi
ya fedha taslimu shilingi milioni moja.
Pamoja na utoaji wa tuzo hizo, hafla
hiyo itasindikizwa na burudani moto moto kutoka kwa wasanii watakaotangazwa
hapo baadaye. Hakuna kiingilio kwenye tuzo hizo bali itatolewa mialiko kwa
baadhi ya watu kwenye tasnia ya burudani na zingine nchini. Pia mialiko 100
itatolewa kwa wananchi waliopiga kura zaidi.
Haya ndio majina yaliyoingia kwenye fainali ya tuzo za watu:
Mtangazaji wa redio
anayependwa
D’Jaro Arungu - TBC FM - TZW1C
Maryam Kitosi – Times FM - TZW1D
Millard Ayo – Clouds FM - TZW1E
Kipindi cha redio
kinachopendwa
Amplifaya – Clouds FM - TZW2B
Hatua Tatu – Times FM - TZW2C
Papaso – TBC FM - TZW2D
Mtangazaji wa runinga anayependwa
Abdallah ‘Dullah’ Ambua – EATV -
TZW3A
Salama Jabir – EATV/Maisha Magic -
TZW3B
Salim Kikeke - BBC Swahili - TZW3C
Kipindi cha runinga kinachopendwa
In My Shoes – EATV - TZW4B
Mkasi – EATV - TZW4C
Planet Bongo – EATV - TZW4D
Blog/Website inayopendwa
Hassbabytz.com - TZW5C
Millardayo.com - TZW5D
timesfm.co.tz - TZW5E
Muongozaji wa video anayependwa
Adam Juma - TZW6B
Hanscana - TZW6D
Nisher - TZW6E
Muongozaji wa filamu anayependwa
JB - TZW7A
Leah Mwendamsoke - TZW7B
Vincent ‘Ray’ Kigosi - TZW7D
Muigizaji wa kike wa filamu
anayependwa
Jacqueline Wolper - TZW8C
Riyama Ally - TZW8D
Wema Sepetu -
Muigizaji wa kiume wa filamu
anayependwa
Hemedy PHD - TZW9A
JB – TZW9B
King Majuto - TZW9C
Mwanamuziki wa kike anayependwa
TZW10
Lady Jaydee - TZW10A
Linah - TZW10B
Vanessa Mdee - TZW10E
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba - TZW11A
Barnaba - TZW11B
Diamond Platnumz - TZW11C
Filamu inayopendwa
Chausiku - TZW12A
Kigodoro - TZW12B
Madam - TZW12C
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/
Ommy Dimpoz - TZW13C
Wahalade - Barnaba - TZW13D
XO – Joh Makini - TZW13E
Kupiga kura andika code ya jina
ulipendalo na tuma ujumbe wa simu kwenda namba 15678 au tembelea
www.tuzozetu.com.
Tags
MATUKIO.BURUDANI