WANAFUNZI ACHENI KUVUTA BANGI MASOMONI : KIMBAU ALONGA


KATIBU wa wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM ,mkoa wa Arusha,Mayasa
Kimbau,amewataka wanafunzi  kuzingatia kilichowapeleka masomoni na
kuacha kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji wa
bangi.

Kimbau alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye
mahafali ya 24 ya  chuo cha Ualimu na ufundi stadi Sinoni ,ambapo
jumla ya walimu 90 wahitimu masomo ya ngazi ya cheti na kutunukiwa
vyeti.

‘’Hivi sasa wanafunzi wengi wanapokuwa masomoni wengi wao wamekuwa
wakijihusisha na makundi ya ajabu na kujikuta wakisahau
kilichowapeleka na wengi wao wakijitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa
za kulevya na uvutaji wa bangi’’alisema

Aliongeza kwa kuwataka wanafunzi na wanavyuo  ,kuwa na uchungu wa
fedha za ada zinazotolewa na wazazi wao wanaowasomesha  na wajikite
kwenye ubunifu wa kuanzisha miradi kwa lengo la kujiajiri kwani suala
la ajira serikalini bado ni ngumu.

Pia alitoa rai kwa wahitimu kuzingatia maadili katika shughuli zao
huku wakijua wazi kuwa wao ni kioo cha jamii na wasibweteke na elimu
walioipata bali wajiendeleze zaidi .

Awali mkurugenzi wa chuo hicho,Edward Laizer,alitoa rai kwa kuiomba
serikali ibadili mitaala na kuweka mtaala wa kujasiliamali .

Alisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na soko la ajira kwa nchi za
afrika mashariki tofauti na sasa ambapo wahitimu wengi hapa nchini
wamekuwa wakikosa ajira kwenye nchi hizo baada ya kumezwa kielimu.

Akizungumzia ufanisi wa chuo chake alisema hadi sasa jumla ya wahitimu
96,000 wamehitimu katika chuo hicho na matawi yake hapa nchini huku
baadhi ya wahitimu wakipata ajira mbalimbali.

Aidha alisema changamoto kubwa inayowakabili wahitimu wengi ni suala
la ukosefu wa ajira hivyo alisema iwapo serikali itabadili mtaala na
kuweka suala la ujasiriamali ,suala hilo linaweza kuwa historia hapa
nchini.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post