Ticker

6/recent/ticker-posts

MFANYABIASHARA MAARUFU WA ,MADINI KIZIMBANI


MFANYABIASHARA maarufu wa Madini ya Tanzanite mkazi wa jijini
hapa,Eliakimu Daud Molle(45),amepandishwa kizimbani katika mahakama
ya hakimu mkazi Arusha akikabiliwa na shitaka la kujipatia madini  ya
thamani ya shilingi milioni 15 kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma mashtaka mwishoni mwa wiki, mbele ya hakimu wa mahakama
hiyo,Nestory  Baro,mwendesha mashtaka wa serikali,Gaudencia Lyimo
aliieleza mahakama hiyo kwamba, mshtakiwa alitenda kosa hilo januari 4
mwaka huu katika jengo  la Ottu, huku akifahamu  wazi kuwa ni
kinyume cha sheria .

Alisema mshtakiwa huyo alijipatia  madini ya Tanzanite  kutoka kwa
mlalamikaji ,Banai Shininu yenye thamani  ya shilingi milioni 15.




Ilidaiwa kuwa mfanyabiashara Mollel alimrubuni mlalamikaji kuwa
anaenda kuuza na baadae angemletea kiasi cha shilingi milioni 15,ikiwa
ni thamni ya madini hayo, hatua ambayo hakufanya hivyo badala yake
alitoweka kusikojulikana.




Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na
mlalamikaji na punde anapopatikana hutoa ahadi za uongo kuwa angelipa
kiasi hicho cha fedha lakini hakufanywa hivyo hadi alipokamatwa na
kufikishwa mahakamani.




Baada ya kusomewa shtaka hilo la kujipatia mali kwa njia ya
udanganyifu,mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo .




Hata hivyo hakimu Baro alimweleza mshtakiwa kwamba  dhamana ipo wazi
kwa masharti ya kuwa na fedha tasilimu kiasi cha  shilingi milioni
7.5,na wadhamini wawili wanaofahamika hatua ambayo mshtakiwa
alishindwa kutimiza na kulazimika kwenda magereza.




Kesi hiyo namba  88 ya mwaka huu, imepangwa kutajwa tena mahakamani
hapo januari 26 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments