Baadhi
ya Mdiwani wa jiji la Arusha wakiongozwa na Meya wa jiji hilo Gaudence
Lyimo kulia ,wakiwa wamebeba jeneza la Belina Kabuje ambaye alikuwa
diwani wa viti maalumu jijini Arusha kuelekea katika katika kanisa la
Parokia Mtakatifu ngarenaro jijini hapa jana
Kushoto ni mtia nia ubunge jimbo la Arusha Filemon Mollel akiwa katika ibada hiyo pamoja na wadau wengine wa CCM
Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha mjini Felix Mrema akisalimiana na akinana waombolezaji waliofika katika kanisa hilo jana
Baadhi
ya vijana wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM(Uvccm) wilayani Arusha
wakibeba mwili wa marehemu Belina Kabuje ambaye alikuwa diwani wa viti
maalumu jijini Arusha kuelekea katika eneo la mazishi eneo la Oljoro nje
kidogo ya jiji la Arusha jana
Mgombea
anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju
ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris ,pembeni yake
akiwa na msaidizi wake Alhaji Kassim Mamboleo wakiwa katika ibada hiyo
jana
Mazishi
ya diwani wa viti maalumu jijini Arusha,marehemu Belina Kabuje ambaye
alifariki hivi karibuni katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi
jana yalitawaliwa na huzuni na hisia mbalimbali mara baada ya familia ya
marehemu kuzuiwa isipokee fedha za rambirambi.
Fedha
hizo zilizuiwa na meya wa halmashauri ya jiji la Arusha,Gaudence Lyimo
wakati akitoa salamu za rambirambi ndani ya kanisa Katoliki Parokia ya
Roho Mtakatifu Ngarenaro wakati mwili wa marehemu ulipofikishwa kwa
ajili ya ibada.
Akizungumza
wakati akitoa salamu hizo bila kutaja kiasi chake meya huyo alisema
kuwa fedha zote zilizokusanywa kama rambirambi ya marehemu
hazitakabidhiwa mbele ya familia yake hadi pale utaratibu wa kufungua
akiba utakapokamilika.
Alisema
kuwa lengo la kuweka utaratibu huo ni kuepusha matumizi mabaya ya fedha
hizo kutumika hovyo huku akisisitiza ya kwamba marehemu enzi za uhai
wake alikuwa mtu mwenye hofu na mashaka .
“Marehemu
enzi za uhai wake alikuwa na hofu sana kuna mambo mengine yalikuwa ni
siri kwa familia lakini alilazimika kutushirkisha sisi madiwani”alisema
Lyimo
Hatahivyo,katika
hali isiyo ya kawaida baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kanisa hapo
walijikuta wakipiga makofi kushangilia hotuba ya meya huyo pale
alipotamka ya kwamba mali za marehemu huyo kamwe hazitaguswa na mtu
yoyote kwa kuwa kuna wosia umeachwa na marehemu.
Naye,mwenyekiti
wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT) mkoani Arusha,Flora Zelothe
aligusa hisia za watu kanisani hapo mara baada ya kutamka kwamba
marehemu aliacha wajukuu watatu ambao alikuwa akiwahudumia na kudai
kimsingi wanapaswa kutambuliwa na familia.
Hatahivyo,paroko
wa kanisa hilo,Anchi Mpota akiendesha ibada ya kumuombea marehemu huyo
aliwataka watu kuondoa tofauti zao za kidini,kikabila na kisiasa kwa
madai kwamba zitawagawa.
“Kwa
hali ilivyo sasa amani tuliyonayo tusiichezee tuondoe tofauti zetu za
kidini,kisiasa na kikabila kama tukiziendekeza basi zitatugawa”alisema
paroko huyo