Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati)
akiambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye
ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (kushoto) walipotembelea shule msingi
Mitindo ya watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio iliyopo katika
wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kulia ni Mtaalamu wa
Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO Tanzania, Bi. Annica Moore.(Picha
zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog
team
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, Zulmira Rodrigues
amesisitiza umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ulemavu wa ngozi katika
jamii baadala ya kuwatenga .
Zulmira alisema hayo alipotembelea watoto wenye ulemavu
wa ngozi katika shule ya msingi ya Mitindo iliyopo katika wilaya ya
Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza mwishoni mwa
juma
Shule
hiyo ya serikali ina wanafunzi zaidi ya 1000 wakimo wenye ulemavu 202
.
Kati
yao 81 ni wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wanahifadhiwa na serikali
katika shule hiyo maasa 24 kufuatia wimbi la mauaji la watu wenye ulemavu
wa ngozi katika mikoa ya kanda ya ziwa .
Hata
hivyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania alionekana kupatwa
huzuni kubwa kutokana hali ya maisha ya watoto hao .
"
Nimehuzunika sana (I am so sad). Sio tabia ya watu wa Afrika kuwatenga watu
wanyonge (weak people)"alisema huku akitokwa na machozi mara baada ya
kuwatembelea watoto hao na kuongea nao pamoja na uongozi wa shule
hiyo.
Alisema ni muhimu watoto hao wenye ulemavu wa ngozi kuwa
wanavaa nguo za mikono mirefu ili kuwakinga na jua kwa ajili ya kulinda
afya zao.
Hata
hivyo Zulmira alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania
kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kutoa wito kwa wadau wote kuunga
mkono juhudi hizo.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini
kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu msingi Mitindo iliyopo katika wilaya
ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Katika
ziara hiyo, Zulmira alikuwa amefuatana na mbunge wa viti maalum
anayewakilisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) Mh. Al shaymaa
Kwegyir.
Mbunge
huyo pia alisema kitendo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kukosa malezi
na mapenzi ya wazazi ni changomoto kubwa iliyopo kwa
sasa.
Alisema ni jukumu la watu wote kulinda na kusadia
kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
"Ufumbuzi wa matatizo ya wetu wenye ulemavu wa ngozi sio
kazi ya serikali tu, ni jukumu la kila mtu",mbunge huyo
alisisitiza.
Aliahidi kuwasilisha bungeni baadhi ya changamoto
zinazowakabili wanafunzi walemavu waliopo katika shule hiyo ya
Mitindo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kurwa Ng'hwelo alisema
serikali inatumia zaidi ya shilingi milioni 10 kuwa ajili ya mahitaji ya
chakula kwa wanafunzi wote wenye ulemavu wapatao 202 kila
mwezi.
Shule
hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wanaosadia wanafunzi hao
walemavu.
Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo
akitoa maelezo ya idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hapo
ambao ni 202 huku 81 wakiwa na albinism kwa Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira
Rodrigues (kushoto) aliyetembelea shule hiyo kuangali changamoto
zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo
akimwonyesha mazingira ya eneo la shule hiyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira
Rodrigues aliyeambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu
wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana
na baadhi ya wanafunzi wa kutwa wanaosoma katika shule ya msingi Mitindo
mara baada ya kuwasili shuleni hapo akiwa ameambatana na Mbunge wa viti
maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa
Kwegyir.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza
na wanafunzi hao waliofurahia ujio wake.
Pichani ni moja ya jengo lililojengwa na Ubalozi wa
Japan nchini Tanzania.
Mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism)
akitoka bwenini kuelekea chumba maalum kwa ajili ya kujipatia chakula cha
mchana katika shule ya msingi Mitindo huku akionekana kutembea kwenye jua
kali pasipo na kuwa na nguo ndefu ya kufunika hadi mikononi kujikinga na
mionzi ya jua inayopelekea kupata saratani ya
ngozi.
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism) ambaye jina
lake halikuweza kupatikana kiurahisi akila chakula cha machana huku
akijikuna kutokana na maumivu makali anayosikia ya majeraha ya mionzi ya
jua iliyoharibu mikono yake na kubadilika rangi ambayo athari yake baadae
ni saratani ya ngozi.
Na
hii ndio hali halisi ya binti huyu katika mikono yake kutokana na kutembea
kwenye jua bila kusitiri mikono yake na nguo ndefu.
Baadhi ya watoto wa bweni wenye Albinism wakijipatia
chakula cha mchana jikoni.
Mtoto mwingine aliyeathiriwa na mionzi ya jua miguuni
na kupelekea kubadilika rangi kuwa mwekundu kutokana na kukosa nguo ndefu
za kujisitiri na mionzi ya jua... wakiendelea kujinoma na chakula cha
mchana.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akionyesha
uso wenye huzuni kubwa kutokana na mazingira magumu waliyonayo watoto hao
shuleni hapo. Kushoto ni Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu
wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir aliyeambatana na Bi. Zulmira
Rodrigues kutembelea shule hiyo. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya
msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mitindo,
Kalunde Cosmas alipofanya ziara fupi ya kutembelea shule hiyo na kujionea
changamoto zinazowakibili watoto wenye ulemavu wa ngozi
(Albinism).
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye
ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akimwonyesha mwandishi wa modewji blog (hayupo
pichani) majeraha ya kuungua na jua kwa mmoja wa watoto mwenye albinism
shuleni hapo.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza
jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyekuwa akijipatia chakula cha
mchana.
Mdau Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha
mchana mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo
wa wazazi wake kwa kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika
shuleni hapo.
Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye
ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule
ya msingi Mitindo alipowatembelea na Bi. Zulmira
Rodrigues.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akisaidiana na Mdau Semeni Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa
shule ya msingi Mitindo.
Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO,
Bi. Annica Moore aliyeambatana na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues
(hayupo pichani) akifurahi jambo wakati akigawa zawadi ya juisi mmoja
watoto wenye albinism shuleni hapo.
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Zulmira Rodrigues akiendelea na zoezi la ugwaji zawadi ya juisi kwa watoto
wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio wa shule ya msingi Mitindo iliyopo
katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza alipowatembelea
mwishoni mwa juma akiwa ameambata na Mbunge wa viti maalum
CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (hayupo
pichani).
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa macho wakijumuika
na wenzao wenye ulemavu wa ngozi na masikio kujipatia chakula cha
mchana.
Mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism anayeonekana
kukosa lishe bora inayostahili kutokana na umri wake ambapo modewjiblog
imebaini kuwa mtoto huyu ana "Utapiamlo" kutokana na kukosa lishe hiyo
bora. Dalili moja wapo ni tumbo lake kuwa kubwa na
gumu.
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akimnywesha juisi mtoto mdogo kuliko wote anayelelewa kwenye shule ya
msingi Mitindo ya watoto wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi,
macho na masikio alipofanyia ziara fupi mwishoni mwa juma mkoani
Mwanza.
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akimnyeshwa juisi mtoto menye ulemavu wa macho alipotembelea shule ya
msingi Mitindo iliyopo wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la
Mwanza.
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akiwa na uso wa huzuni kutokana na mazingira ya watoto hao na kupelekea
kumwaga machozi kwa uchungu yeye kama mama mwenye kuthamini upendo. Kushoto
ni Mh. Al Shaymaa Kwegyir.
Bw. Abdulaziz Mbegele wa kitengo cha Logistic kutoka
UNESCO, akimnywesha juisi mtoto mwenye ulemavu wa macho wakati wa ziara
hiyo na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO nchini
Tanzania.
Mtoto alyefahamika kwa jina moja tu Kevin mwenye umri
wa miaka 11 ambaye alifikishwa kwenye shule hiyo akiwa mdogo sana na wazazi
wake kumtelekeza hadi leo huku akiwa hamjui mama, baba, mjomba, dada, kaka
wala shangazi..... kisa amezaliwa na albinism....!
Mtoto Kevin akipata "self" na mjomba wake mpya Zainul
Mzige wa modewjiblog
aliyeambatana na ugeni huo.
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akizungumza na waandishi wa habari na kutoa hisia zake kuhusiana na
changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa nguvu na kusisitiza
upendo kwa watu wenye albinism.
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye
ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani).
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia