Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa kipindi cha miaka 15 kwa tiketi wa CCM,Elisa Mollel akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kuwa Mbunge jimbo la Magharibi
Mwaandishi
wa habari mwandamizi wa gazeti la Mwananchi kulia Mosses Mashala
akifanya mahojiano na aliyewahi kuwa mbunge jimbo la Arumeru Magharibi
Elisa Mollel,kulia ni anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini Victor
Njau
"Elisa Mollel anasema yuko fiti kiafya na kuhusu watu kusema kuwa ni mgonjwa ni propaganda tu sasa kuingia ulingoni kupambana"
Aliyewahi
kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa tiketi wa CCM,Elisa
Mollel ametamka ya kwamba atatangaza uamuzi wa kugombea jimbo hilo au la
pindi muda utakapowadia kwa kuwa ana uzoefu mkubwa na siasa za jimbo
hilo.
Mbali
na kauli hiyo Mollel amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifuatwa na
makundi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa mila maarufu kama
Malaigwanani,viongozi wa dini,wakinamama wakimshawishi agombee ubunge
mwaka huu.
Hadi
sasa makada mbalimbali kupitia CCM wilayani Arumeru Magharibi
wametangaza nia ambao ni Mathias Manga,Robinson Meitinyiku,Thomas Ole
Sabaya pamoja na mbunge wa sasa wa jimbo hilo,Goodluck Ole Medeye.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi jijini Arusha Mollel alisema kuwa tangu
alipong”atuka katika utumishi wake baadhi ya wananchi wilayani humo
wamekuwa wakimfuata na kumtaka achukue fomu kwa madai mambo hayaendi
sawa.
“Wananchi
wananifuata na kuniambia mzee mambo ni hovyo tangu
ulipoondoka,nimefuatwa na makundi mengi tu na mimi nasema muda ukifika
nitasema jambo”alisema Mollel
Hatahivyo,alisisitiza
ya kwamba tangu ang”atuke miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa
yakimsikitisha ni pamoja na ubovu wa miundombinu,kero ya maji sanjari na
kero ya migogoro ya ardhi matatizo aliyodai yameshindwa kutatuliwa na
mrithi wake.
Hatahivyo,alisema
kuwa miongoni mwa mambo ambayo anajivunia hadi sasa ni pamoja na rekodi
yake ya kuboresha sekta ya elimu wilayani humo ambapo aliondoka huku
akiwa amefanikiwa kuacha shule za sekondari 26 tofauti na alipoingia
madarakani.
“Hapo
awali tulikuwa na watoto wengi sana wanamaliza elimu ya msingi lakini
hawaendi sekondari nimeondoka na kuacha shule za sekondari 26 katika
kila kata najivunia kwa hili”alisema kwa kujiamini