Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana
na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa
(TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati
wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki
mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika
katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).(Picha zote na Zainul
Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog
team
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (TAMISEMI),
Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi katika kumwezesha
mtu kujitegemea.
Kauli
hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog kuhusu maendeleo na
changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki ya maadhimisho ya elimu
inayofikia tamati leo mjini Dodoma.
Alisema katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa
unawaondoa watu kwenye ajira ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji
wa elimu ndio kitu cha msingi kabisa.
Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza
usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu
nchini.
Alisema kuna mambo mengi ambayo yanastahili kuangaliwa
kwa sasa kutokana na vigezo vya ufanisi wa elimu kuonesha changamoto
zinazokabili sekta hiyo pamoja na kuimarika kwake.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupungua kwa
uandikishaji wa watoto na mdondoko.
Alisema viongozi, wazazi pamoja na walezi wamesahau
wajibu wao na kumwachia mwalimu pekee katika kumlea mwanafunzi kimasomo na
hii ndio chanzo kikubwa cha mdondoko na ufaulu mbaya.
Alisema ni vyema watu wakajiuliza hawa wanaondoka
wanakwenda wapi na wanafanya nini.
"kuna
sheria ambapo viongozi wa kata wanaruhusiwa kuwachukulia hatua na
kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokwamisha elimu, lakini watu hawachukia
sheria hiyo" alisema.
Aidha
alisema ubora wa elimu una vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kujituma kwa
walimu katika ufundishaji na kuwa na dhamira ya kuwapa watoto vitu vyenye
maana.
Alisema kuna mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuinua elimu
na usimamizi unapokuwa mkali na wahusika kuadhibiwa ndio ufanisi
unafanyika na mdondoko kuangaliwa.
Alisema ipo haja kubwa ya kuwekeza kwenye elimu kwa
viongozi na wadau kutimiza wajibu wao.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi , Makuru Petro akitoa tathmini ya sekta ya elimu kwa
wadau wa sekta ya elimu alisema pamoja na ongezeko la ufaulu ndani ya miaka
miwili ipo haja ya kutathimini uimara wa mfumo katika kutoa huduma ya
elimu.
Alisema pamoja na ufanisi kuwapo kwa idadi kubwa ya watu
wanaokacha shule kunaonesha mfumo kuwa na kasoro na lazima
uangaliwe.
Aidha
alisema sekta ya elimu wamepokea asilimia 97 ya bajeti yake na kwamba
asilimia 70 imeenda kwenye halmashauri ambako ni watekelezaji wa miradi ya
elimu.
Tathmini hiyo inayowakilisha wizara zote
zinazoshughulikia elimu kama TAMISEMI, Elimu na Maendeleo ya jamii na wadau
wengine wa elimu ni sehemu ya shughuli inafanywa kila mwaka kwa lengo la
kutambua kilichofanyika, changamoto na namna ya kukabiliana na tatizo
hilo.
Hata
hivyo walisema kwamba ndani ya miaka miwili kumekuwepo na maendeleo
makubwa katika sekta ya elimu hasa ufaulu na ubora wa
elimu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto)
mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
(kulia) akimweleza yaliyomo kwenye taarifa ya ripoti ya hali ya Elimu
ilivyo dunia (EFA Global Monitoring Report 2015) "Education For All
2000-2015" ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto kidunia iliyoandaliwa
na Shirika la UNESCO alipomtembelea ofisini kwake Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini
(kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja mjini Dodoma ambapo pia
alikutana na wadau wa sekta ya elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini
sekta ya Elimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
akimwonyesha takwimu za Tanzania zilizomo kwenye ripoti hiyo Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI),
Jumanne Sagini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na.
Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) akiuliza swali kwa
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mazungumzo
ofisini kwake mjini Dodoma.
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa
UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la UNESCO, Zulmira Rodrigues (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI),
Jumanne Sagini (kushoto) katika ofisi za TAMISEMI mjini
Dodoma.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia