Ticker

6/recent/ticker-posts

LOWASA ACHANGISHA MILIONI 234 UJENZI WA SHULE LEO


 WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
Na Woinde Shizza,Arusha
WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ameongoza harambee ya kuchangia
ujenzi  wa shule  ya sekondari na kufamikiwa kuvuka malengo kwa
kuchangisha  kiasi cha shilingi milioni 234.5,huku malengo yakiwa ni
shilingi milioni 200.
Aidha fedha hizo zitafanikisha ujenzi wa  jengo la ghorofa tano kwenye
msikiti wa Patandi uliopo Tengeru ambalo mpaka kukamilika kwake
itagharimu shilingi bilioni 2.
Kwenye harambee  hiyo  kiasi cha shilingi milioni 105 ni mchango wake
pamoja na Makamu wa Rais na marafiki zao.
Lowassa alisema kuwa alipopewa taarifa ya kumwakilisha Makamu wa Rais
kwenye harambee hiyo aliogopa kwani kuna maeneo na misikiti kadhaa
waliyomuomba akafanye hivyo lakini hakuweza kwenda kwani alikuwa
kwenye kifungo ndani ya chama chake.
"Na nimefurahi nimekuja wiki moja kabla ya jambo dogo tu niwaambieni,
wiki ijayo tarehe 24 ya mwezi huu ninakuja hapa uwanja wa Sheikh Amri
Abeid, nataka nije niseme neno, nitasema neno ambalo nitawaomba
mniunge mkono...
" Sitaki kuhatibu uhondo wa tarehe 24 jiandani mje, na nitaka kila
mwana Arusha ajitokeze na akikuuliza mtu unakwenda wapi mwambie
ninakwenda kwenye safari ya matumaini," alisema Lowassa.
Alipongeza namna harambee hiyo ilivyoandaliwa ikiwashirikisha watu wa
dini, makabila na rangi tofauti jambo alilosema kuwa ni la kuenziwa
kwani linadumisha Utaifa zaidi.
Kwenye harambee hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali
wakiwemo Wakuu wa wilaya ya Arusha, Christofa Kangoye na Arumeru,
Hasna Mwilima, madiwani na wabunge huku watia nia ya ubunge kupitia
CCM wakitumia fursa hiyo kujinadi kwa kutoa michango mikubwa.
Lowassa alisema kuwa yeye na Makamu wa Rais Dkt Bilal na marafiki zao
wanatoa  fedha taslim sh milioni 50 ambapo sh milioni 55 ni ahadi huku
wananchi wengine wakichangia fedha taslim sh milioni 17.
Awali Katibu wa Bakwata mkoani hapa, Sheikh, Shaban Juma alisema kuwa
msikiti wa Patandi ulianzishwa mwaka 1997 ambapo kwa sasa mahitaji
yameongezeka hivyo wanahitaji kufanya upanuzi kwa kujenga jengo la
ghorofa tano ambalo katika awamu ya kwanza wanahitaji sh milioni 200.
Alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili yakujenga msingi na ghorofa ya
kwanza ambapo wao tayari walisha changishana fedha na vifaa vyenye
thamani ya sh milioni 90.

Post a Comment

0 Comments