Waliofanikiwa kufika kilele
cha Shira hawakusita kuonesha furaha zao kwa kucheza .
IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya
Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani
ya kipindi cha miaka 10 huku
asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni wazawa.
Asilimia hiyo
inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda
Mlima huo kwa muda wa siku moja hali
inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi
zetu ili kujionea urithi tuliopewa
na Mungu.
Mhifadhi utalii wa KINAPA,Eva Mallya alisema
katika kuhamasiosha utalii wa ndani
,KINAPA imeandaa zoezi maalumu ambalo litadumu kwa muda wa siku nne kwa watanzania walio walio karibu
na mlima kuweza kuupanda kwa muda wa siku moja na
kurudi.
"Tumeandaa zoezi rahisi kwa kila mmoja mwenye
nafasi aweze kupanda,sehemu
kubwa itakuwa ni kwa kutumia gari ambapo walio
tayari watachukuliwa na gari hadi eneo
fulani kabla ya kutembea umbali mdogo na kutizama uwanda wa Shira katika mlima
Kilimanjaro."alisema Mallya.
Alisema zoezi la
uandikishaji kwa ajili ya watakao penda kupanda katika mlima huo tayari limeanza katika vituo
vilivyoko jirani na Duka la Maua
mkabala na Rafiki Supermarket ,Hosptali ya rufaa ya KCMC
na njia Panda ya Himo.
Mallya alisema mpandaji atapaswa kujitegemea kwa
Sweta na Jacket kwa ajili ya baridi
,suruali raba pamoja na chakula huku mhusika
akitakiwa kulipia kiasi cha
sh 15,000 kama kiingilio cha hifadhini.
Kwa upande wake afisa masoko wa KINAPA,Antypas
Mgungusi alisema safari ya kupanda
mlima Kilimanjaro imekuwa ikitumiwa na baadi ya
watalii kufanya matukio ya kihistoria
ikiwemo kufunga ndoa na wengine kuadhimisha siku zao za kuzaliwa wakiwa
kileleni.
"Imezoeleka kuwa watu wanapokuwa na matukio yao
yakiwemo ya mikutano,au Honey
moon baada ya ndoa na siku za kuzaliwa wamekuwa wakifanya sherehe zao mijini,lakini kuna maeneo
mengine kama haya ya hifadhi kufanyia mambo hayo"alisema
Mgungusi.
Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu
duniani kwa kuhifadhi barafu kwa
kipindi cha mwaka mzima licha ya kupitiwa na mstari
wa Ikweta huku ukiwa ndio mlima
pekee uliosimama peke yake ukilinganisha na milima mingine
duniani.
|