Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta
akicheza sambamba na Mkurugenzi wa kituo cha Radio 5 Robart Francis
staili ya shikorobo juzi kwenye party ya usiku wa marafiki wa Lowassa
ulifanyika katika ukumbi wa triple A jijini Arusha
Kundi la marafiki wa Lowasaa chini ya umoja wao unaojulikana kama “4 U Movement”wakishangilia katika party hiyo
Katibu mwenezi wa CCM mkoani Arusha, Isack Joseph maarufu kama “kadogoo”akicheza na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta
katika party ya usiku wa marafiki wa Lowassa uliofanyika katika ukumbi
wa Triple A jijijni Arusha nakuhudhuriwa na watu mbalimbali
Kada maarafu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mfuko akishow love na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta katika usiku wa marafiki wa Lowassa iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha
Wacheza show wakiwa wanafanya yao stejini
Mwanabloga wa libeneke la kaskazini Woinde Shiza akishow love na Deo Gee mfanyakazi wa kituo cha Radio 5 jijini Arusha
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta na
mwenzake,Abdulwaheed Sykes”Dully Sykes”wikiendiiliopita wametangaza rasmi kumuunga
mkono mgombea anayetajwa kuwania nafasi ya urais kupitia CCM mwaka
huu,Edward Lowasa.
Wasanii
hao walitangaza uamuzi wao katika ukumbi wa burudani wa triple A uliopo
jijini Arusha wakati walipokuwa wakiburudisha onyesho la marafiki wa
Lowasa maarufu kama”Friends of Lowasa white Party”.
Akitangaza
uamuzi wake,Sykes alisema kuwa yeye amemua kumuunga mkono Lowasa katika
mbio za urais kwa kuwa ndiye chaguo lake tangu hapo zamani.
“Jamani
mimi namuunga mkono Lowasa yeye ndiye chaguo langu tangu zamani mimi ni
mfuasi wa kiongozi huyu”alisema msanii huyo na kuibua shangwe
Hatahivyo,kwa
upande wake Billal alisema kuwa yeye atamuunga mkono mgombea huyo
anayetajwa kuwania nafasi ya juu katika medani za siasa hapa nchini endapo akipitishwa na chama chake.
Alisema kuwa kila binadamu ana mapenzi yake na kwa maana hiyo yeye atamuunga mkono Lowasa kwa kuwa ndiye changuo lake kwa sasa.
Katika
onyesho hilo lililoanza majira ya saa 10.00 usiku watu mbalimbali kabla
ya kuwasili ukumbini walipata fursa ya kupiga picha katika zulia
jekundu ambapo usiku huo ulipambwa na vazi jeupe ambapo watu mbalimbali
walivalia vazi hilo.