Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo wanasema kuwa watu ishirini na watatu wameuawa kikatili na
wanaodaiwa kuwa waasi wa Uganda.
Wanane kati ya waliofariki ni wanajeshi wa DRC.
Shambulizi hilo lilifanyika Jumatano usiku.
Waasi
wengi wao wakiwa wa Allied Democratic Forces (ADF) wamefanyana
mashambulizi kadhaa kusini mwa mji wa Beni katika siku za hivi karibuni.
Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda walifanya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vinavyokiuka ubinadamu.
ADF imewaua mamia ya watu wakati mwingine na ndo, panga na visu.
chanzo bbc news
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia