Kundi la muziki la Tip Top Connection
limethibitisha kufanya collabo na rais wa Wasafi Classic, Diamond
Platnumz katika wimbo uitwao ‘Kinanukaga’.
Akiongea Madee amesema kuwa kazi hiyo
ambayo imekamilika kwa asilimia 80 itatoka mwezi ujao lakini kabla ya
kazi hiyo kutakuwa na kazi kadhaa za utangulizi kutoka kwa members wa
Tip Top Connection.
Madee ameongeza kuwa kundi hilo sasa
linajikita zaidi katika kutangaza muziki wao nje ya nchi hivyo lazima
wafanye kazi nzuri na za kuvutia kwa mashabiki wa muziki wao.