Mwl. Samwel Tupa
Wanariadha
wa kimataifa Michael Gwandu na Michael Michael Danford wa Arusha wameanza
mazoezi makali ya kuhakikisha wanavunja rekodi ya kitaifa za mbio fupi, ya
kuruka chini na viunzi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa.
Wanariadha
hao wanaojifua katika viwanja vya sheik amri abeid kwa kuruka viunzi na kuruka
chini na mitupo wamesema kuwa wamekuwa mabingwa wa mchezo huo kwa miaka zaidi
ya tano sasa hivyo kwa sasa mwaka huu wanajifua kwa ajili ya kuvunja rekodi ya
taifa ya michezo hiyo.
“Sisi tunajinoa makali kwaajili ya kuvunja rekodi za kitaifa kwanza
na baadae dunia katika mbio fupi, kuruka na mitupo ambapo mbali na kuwashinda
wapinzani wetu wa mikoa mingine lakini pia ni kuvunja rekodi ya kitaifa
zilizowahi kuwekwa ikiwemo ya kuruka chini iliyowekwa na Raphael Mlewa mwaka
1971”
Kwa upande wa kocha wa wanariadha hao Samweli Tupa alisema
kuwa wanariadha hao wamekuwa wakichukua ubingwa wa mara kwa mara katika mashindano
ya kitaifa na jumuiya ya madola lakini cha kushangaza wengi wameshindwa kuvunja
rekodi zilizowekwa kipindi cha nyuma hali ambayo ameamua kuwanoa wachezaji wake
wavunjerekodi hizo.
“Kuna rekodi zimewekwa miaka zaidi ya 40 sasa kama mirujko
mitatu iliwekwa rekodi mwaka 1970 na John Kanondo na kuruka viunzi kwa mita 110
lakini cha kushangaza rekodi hizo hazijavunjwa licha ya kila siku kujisifia
wachezaji wetu kufanya vizuri kwa kuwa wa kwanza wakati rekodi za miaka ya
ukolono bado ipo”
alisema
kuwa kwa sasa wanariadha hao mbali na kufanya mazoezi ya peke yao pia
watashiriki katika mashindano mbali mbali ikiwemo ya may 25 ya kitaifa
itakayochagua wachezaji watakaowakilisha nchi katika mashindano ya wazi
ya Uganda mwezi june.
Hata hivyo kochaTupa aliiomba serikali kusaidia mchezo huo
kama awali ili uweze kuendelea kurudi na medali nyingi na kuvunja rekodi za
dunia kama awali na kusema kuwa Tanzania inashindwa kufanya vizuri kutokana na
kukosekana kwa sapoti kutoka serikalini kama ilivyokwa nchi kama Kenya, Unganda,
n.k.