Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mgwira
(pichani) amesema chama hicho hakina matatizo na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) na hata sasa kinasubiri majibu ya barua yao waliyoituma
kwa umoja huo kuomba kuunganishwa.
Mgwira
alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kilipofanya ziara ya kutembelea
hospitali ya mkoa ya Mt Meru kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya
kinamama ikiwa ni njia ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa
kwake.
Alisema ACT-Wazalendo wanaunga mkono muungano wowote wa vyama vya upinzani nchini ulio halali.
“Hatuna matatizo na Ukawa tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani ulio halali,” alisema kiongozi huyo
Alisema tangu waandike barua ya kuomba mwongozo wa namna ya kujiunga na Ukawa, bado hawajapata mrejesho.
“Tunatamani
kuunganisha nguvu katika siasa za vyama vya upinzani na sasa tunasubiri
majibu ya barua yetu ya kuomba kuingia Ukawa,” .
Alisema
kuwa chama hicho kimepokewa vizuri na wananchi wa mikoa mbalimbali
nchini na katika ziara ya awamu ya kwanza walifanikiwa kuingiza jumla ya
wanachama wapya 700.
“Tumepokewa vizuri mikoani tumefanikiwa kuingiza wanachama wapya na hoja ya umoja na uzalendo watu wameipokea vizuri,” Mgwira.
Akipokea
misaada katika hospitali hiyo Muuguzi Mfawidhi, Sifael Masawe alisema
kwamba misaada hiyo itasaidia kupunguza shida za wagonjwa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia