KCBL YAKUSUDIA KUTOA ELIMU YA KUENDESHA VIKOBA KWA WATEJA WAKE



BENKI ya ushirika mkoani Kilimanjaro (KCBL) inakusudia kutoa elimu na 
namna mbalimbali za kuendesha vikoba ili wanachama waweze kuwa wabunifu wa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kuacha kutegemea vikoba pekee.

Amesema benki ya KCBL itatoa elimu na ushauri kwa wanachama wa vikoba namna ya kuviendesha kuwa wabunifu na kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayowezesha wanachama kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Meneja wa benki ya Ushirika mkoani Kilimanjaro (KCBL),Elizabeth Makwabwe, wakati wakivunja vicoba vyao na kuendesha harambee ya kutunisha mfuko wao.

Alisema wakati wa kuanzisha miradi  wanachama wa vikoba hawana budi kuitofautisha badala ya kuigana kwani kuna miradi ya aina nyingi ambayo ikianzishwa kwa ubunifu na uaminifu itaweza kuwainua wanachama kiuchumi.

Akisoma risala ya wanachama wa kikoba cha Obama, Amina Salimu amesema idadi ya wanachama wake imeongezeka kutoka  wanachama 15  mwaka 2003 hadi kufikia 107 na kwamba kikoba chao kimeweza kuwakopesha wanachama
wake mkopo wa zaidi ya shilingi 33,376,0000 na kina hisa
19,122,000,mfuko wa jamii 5,564,000 riba 3,376,000 .

Amesema lengo la kuanzishwa kwa kikoba cha Obama  ni kuunganisha nguvu za kiuchumi na kuinua kipato cha wanachama wakena kwamba wanaakusudia kununua shamba lenye ukubwa wa ekari hamsini.

Amesema changamoto zinazokikabili kikoba cha obama ni pamoja na ukosefu wa ofisi,vitendea kazi vya kutunza kumbukumbu na kuwa na mtaji mdogo ambao hautoshelezi mahitaji ya wakopaji.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post