anayetoa maelezo ni afisa matekelezo wa NHIF mkoa Arusha, Desderius Buhiye
muongoza watalii Julius Mwenda akiuliza swali juu ya mfuko huo, utakavyowasaidia wakiwa nje ya mkoa. Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya(NHIF), umeshauriwa kuanzisha utaratibu wa kuingia ubia na hospitali za nchi jirani, ili kuwawezesha wanachama wake, kupata huduma bora za matibabu wakiwa nje ya nchi. Wito huo, ulitolewa na wanachama wa chama cha waongoza watalii Tanzania(TTGA),katika semina ya kupatiwa elimu juu huduma za mfuko huo, kuhusiana na fao jipya la wanavikundi. Raphael Njavu alisema, wao kama waongoza watalii wamekuwa wakifanyakazi hadi nje ya nchi, hasa nchi jirani hivyo mfuko huo, utazame uwezeno wa kuingia ubia na hospitali za nje. "kama sio ubia basi NHIF ijitahidi kuboresha hospitali za wilaya za mipakani ni ili wanachama waweze kupata huduma bora badala ya kulazimika kurudi mijini"alisema. Hata hivyo, Afisa matekelezo mfuko wa NHIF mkoa wa Arusha, Desderius Bushiye akijibu hoja hiyo, alisema mfuko huo unaendelea kuboresha huduma za afya na sasa hospitali nyingi hata za mipakani zimekuwa zikitoa huduma za bima. "kwa wale ambao wanasafiri wilaya zote mfuko unatoa huduma na hata Zanzibar kuna hospitali kubwa ambazo zinatoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya"alisema. Alisema mfuko wa Taifa ya bima ya afya, umeanzisha utaratibu wa kuwapa uanachama wanachama wa vikundi, kwa kulipia Tsh 76,800 kwa mwaka ili kuhakikisha watanzania wengi wanakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya popote walipo nchini.
Awali
Katibu Mkuu wa TTGA Emmanuel Mollel alisema wanachama wake, wamekubali
kujiunga na mfuko huo, ili kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya
popote walipo nchini.
"sisi
kama chama tumekubali kujiunga na NHIF na tunauhakika sasa wanachama
wetu watatoa huduma bora kwa watalii wakiwa na afya njema"alisema.
|
habari kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog