Naibu Kamanda wa UVCCM
,Innocent Melleck akiwa na mama mzazi wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima
mara baada ya kukabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa ajili
ya kusaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
Naibu kamanda wa UVCCM
wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akikabidhi Pempers kwa
mama wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima kwa ajili ya kumsaidia mtoto
huyo aliyepata ulemavu wa miguu miwli baada ya kugongwa na gari aina
ya Fuso.
Naibu kamanda wa UVCCM
wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Melleck akiwa amembeba mtoto
Felista Shirima(3) aliyekatwa miguu yote miwili baada ya kugongwa na gari
aina ya Fuso jirani na nyubani kwao.
Akizungumzia sakata la mtoto huyo Naibu kamanda huyo alisema
kuwa
ataumia kila aina ya uwezo na nguvu zake kwa kushirikiana na ofisi ya umoja
wa
vijana wa chama chama mapinduzi UVCCM ili kuhakikisha kuwa haki
ya
mtoto huyo inapatikana.
Awali
akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa
baiskeli ya magurudumu matatu na vifaa mbalimbali vyenye thamani
ya zaidi ya shilingi laki saba na kamanda huyo, mama mzazi wa mtoto huyo
Beatrice
Kelvin,aliiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kumsaida mwanae
ili
kuhakikisha haki inapatikana.
Alisema
kesi iliyokuwepo mahakama kwa ajili ya kudai haki za
msingi za mwanae imeisha bila haki yake kupatikana licha ya kuhangaika
sehemu
mbalimba na kuomba vyombo husika vinavyo jishughulisaha na haki za
binadamu kuingilia kati suala hilo hatua ambayo itasaida kupata
haki.
--