Na Daniel Mbega ,
Mwanza
SHAHIDI wa sita katika kesi
ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Mkaguzi wa Polisi
(Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa ushahidi wake leo hii katika Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza.
Mbele ya Jaji Robert
Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014, shahidi huyo
ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na mawakili wa serikali Emil
Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.
Hata hivyo, Jaji Makaramba
aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya kutokea mgongano wa
kisheria katika masuala ya vidhibiti kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa
upande wa utetezi, hivyo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi
hilo.
Washtakiwa katika kesi hiyo
ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph
maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.
Marehemu Nongo aliuawa Juni
26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini
Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili
na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia