BENKI YA NMB YASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO HAI


BENKI ya NMB kanda ya Kaskazini,imetoa msaada wa vyakula,Magodoro na
Mahema kwa wahanga wa Mafuriko yaliyotokea wilayani Hai  na
kusababisha nyumba  zaidi ya 50 kubomoka na zingine 30 kuweka nyufa
huku watu zaidi ya 200 wakikosa makazi.

Meneja wa benki hiyo Vicky Bishubo alisema msaada huo wenye thamani ya
shilingi milioni 10 ,unalenga kuwasaidia waathirika hao ambao kwa sasa
hawana makazi ya kuishi ,huku akiba ya vyakula walivyokuwa navyo
vikiharibiwa na mvua hiyo, iliyonyesha Mei 2 mwaka huu.

Alisema benki yake imekuwa na sera ya kusaidia mambo matatu ,Afya
,Elimu na Maafa kutokana na faida kidogo inayoipata.

 ‘’ Kwa kutambua umuhimu wa jamii  benki yetu imeona upo ulazima wa
kusaidia jamii yoyote yenye uhitaji na tumekuwa tukifanya hivyo kwa
kuwarejeshea wananchi faida kidogo tunayoipata’’alisema

Aidha alieleza kuwa Benki  hiyo itaendelea kusaidia jamii kupitia sera
hiyo na imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili hiyo.

Alifafanua msaada huo ni pamoja na Maharage kilo 500,Mahindi kilo
2000,Mafuta ya kupikia lita 1000,Sukari mifuko 50,Magodoro 70 na
Blanketi 50.

Kwa upande wa mkuu wa wilaya hiyo,Antony Mtaka alisema mvua hizo
zilizonyesha tarehe 2,zilifanya uharibifu mkubwa ikiwemo kung’oa
reli,kuharibu ekari 450 za mazao mbalimbali na kuharibu miundo mbinu
ya barabara.

‘’Hayo mafuriko yameleta madhara  katika kata tatu za Weruweru,Masama
Rundugai na kata ya mnadani’’alisema

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe alijitolea
kuwajengea nyumba hizo 50 baada ya wananchi hao kupendekeza hivyo
,alipowaomba wachague msaada atakao utoa mbunge.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post