UTAFITI UNAONYESHA KUWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 WILAYA YA MONDULI IMEATHIRIWA NA MMOMONYOKO WA ARDI,WANANCHI WASHAURIWA KULIMA KILIMO HIFADHI

Watafiti kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na Schumacker wakiwa wanamsikiliza kwa makini mkalimani ambaye ni  ndugu Sitayo aliyevaa (miwani ) katika warsha ya Wadau wa Jali Ardhi iliyofanyika Chuo Cha Ualimu Monduli.
 
Wakwanza kushoto ni Profesa Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akiwa anafuatilia kwa karibu Profesa William Blake kutoka nchini Uingereza akipanda mti katika eneo la chuo cha Ualimu Monduli.



Mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akitoa elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili wilayani Monduli.

Mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi akitoa elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili wilayani Monduli.

Profesa Willium Blake akifuatilia kwa makini kinachoendelea katika Warsha hiyo

Zoezi la upandji Miti likiwa likiendelea kwa wageni kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na Schumacker wakishirikiana na Dkt Kelvin Kimei (anayeandika )kutoka  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha 
Pichani Dkt Kelvin Kimei akimuelekeza mmoja wa wageni kutoka nchini Uingereza namna ya kuotesha mti ikiwa ni kumbukumbu ya kutunza mazingira katika Chuo cha Ualimu Monduli.
 Mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi akitoa elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili wilayani Monduli.
 Profesa Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akiwa anatoa ufafanuzi wa jambo katika warsha ya Mradi wa Jali Ardhi kwa wadau waliohudhuria katika Chuo Cha Ualimu  Monduli
 Profesa William Blake kutoka nchini Uingereza akitoa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa warsha ya siku mbili iliyowakutanisha wadau wa Mradi wa Jali Ardhi aliyesimama kushoto kwake ni Charles Bonaventure kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya ECHO




Wananchi wa monduli wameaswa kulima kilimo cha uhifadhi ili kuhifadhi  mazingira na kuepusha kutokea kwa mmomonyoka wa ardhi katika maeneo yao  na kudhibiti makorongo yakiwa katika hatua za awali.


Hayo yamesemwa na  Issakwisa Ngondya mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  Arusha ambapo amesema kuwa zaidi ya asilimia 50 katika wilaya ya Monduli imeathiriwa na mmomonyoko wa ardhi .


 Ameainisha vijiji vilivyoathirika zaidi ni pamoja na Emaerete,Lendikinya,Arkaria,Orchoropus ,Likamba,Oletushora pamoja na Nangungwa,amesema kutokana na uharibifu  huo wa ardhi  umesababisha rutuba kupotea katika ardhi na husababisha upatikanaji hafifu wa mazao kwa mkulima.
  Amewataka wadau hao kuhifadhi uoto  kwa kuotesha mimea na miti ili kuzuia udongo usisombwe na maji au upepo kwani  ardhi iliyofunikwa ni madhubuti zaidi dhidi ya mmomonyoko wa udongo kuliko ardhi ambayo haijapandwa kitu amesisitiza  kupanda mazao ya kudumu na kupanda mazao yanayofunika ardhi. 



Nae Profesa  William Blake  kutoka nchini Uingereza amesema kuwa amefurahishwa sana na matumaini makubwa waliyonayo wana Monduli kwaajili ya kurudisha ardhi liyokuwa imeharibika  kwa mafanikio makubwa kwani warsha hiyo ina umuhimu mkubwa kwa watu wote wa sasa na kwa vizazi vijavyo pia


Kwa upande wake Profesa Patrick Ndakidemi  amesema akiona mashamba yameharibika huwa anajisikia vibaya kwani bila ardhi hakuna maisha amewataka washiriki wote kuyatendea kazi yale yote waliyojifunza ambapo amewataka wadau hao kuwa mfano bora  katika maeneo yao.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya serikali  Afisa kilimo na ushirika na umwagiliaji Ridhiwani kombo kutoka halmashauri ya Monduli amewashukuru waliofanya utafiti na kurudisha majibu kwani wengine huwa wanafanya utafiti lakini hawarudishi majibu,amesema utafiti walioufanya utatumika katika maeneo mengine hapa nchini.
 
 Kwa upande wawashiriki akitoa neno la shukrani katika semina hiyo ya siku mbili Adiso Matayo kwa niaba yawengine amewashukuru wawezeshaji kwa kuwapatia elimu ambayo ni faida kwao na kwa kizazi kijacho amesema elimu waliyoipokea wataifanyia kazi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post