![]() |
Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko akipokea zawadi kutoka kwa moja wa wafanyabiashara wa madini |
Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko akiongea wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha lililozinduliwa rasmi leo |
baadhi ya wafanya biashara wa vito vya madini wakifatilia kwa makini
waziri akiangalia baadhi ya vito vilivyopo katika soko hilo baadhi ya wafanyabiashara wakiangalia vito vilivyopo katika soko hilo
Mwenyekiti wa TAMIDA, Sammy Mollel akiongea katika uzinduzi huo ambapo alishukuru kwa kuanzishwa kwa soko la madini pia alipongeza serikali kwa bajeti ya mwaka
2019/20 kwani imeondoa kilio cha muda mrefu cha wachimbaji na wauzaji wa madini nchini.
mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea katika uzinduzi huo
mbunge wa viti maalumu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge nishati na madini Catherine Magige akiongea katika uzinduzi huo |
Na Woinde Shizza Michuzi
Tv,Arusha
Waziri wa
madini Doto Mashaka Biteko,amewataka wafanyabishara wa madini wadogo
pamoja na wakubwa kuwafichua wafanyabiashara wote wanaojaribu kutorosha
madini pamoja na wale ambao wanaokwepa kulipa kodi ya serikali ili hatua
kali zichukuliwe dhidi yao
Hayo ameyasema leo
wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha ,ambapo alisema kuwa
Iwapo wafanya
biashara watakuwa wawazi na watafichua watu wote ambao wanakwepa kodi na
kutorosha madini hitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi yetu.
Alisema kuwa
ili kuweza kuinua uchumi wan chi yetu ni lazima kila mwananchi kutimiza wajibu
wake kwa kulipa kodi kwa uaminifu ili kusaidia kukuza uchumi wan
chi yetu aidha alisisitiza kuwa heshima kubwa ya mtanzania ni kulipa kodi na
sio kufanya mambo ya kijanja janja na alibainisha kuwa ni lazima watanzania
tuhame katika taifa la watu wajanja wajanja tuwe wananchi wa taifa la watu
waaminifu .
“mlilalamika
kuhusiana na kodi tumefanyia kazi na yale ambayo bado tutafanyia kazi
lakini kwa kuwa tumefanyia kazi na nyie rudisheni fadhila kwa kulipa kodi ,na
pia napenda kuwasihi wenyeviti wa mabroka kuwakusanya mabroka ambao hawajalipa
kodi kulipa kodi wakate leseni ili nao wawe katika orodha ya walipa
kodi”alisema Biteko
Alibainisha
kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa
ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha
watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa
Aliendelea kueleza
kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa
wafanyabiashara wa madini hususani wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo
hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya
zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.
Alibainisha kuwa
kuwekwa kwa soko hili hapa Arusha kunasaida kuwepo kwa mazingira mazuri
ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali
zinazofikia asilimia 23 na pia soko hili litasaidia kuondoa utoroshwaji wa
madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa.
Alieleza manufaa
mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za
wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.
“napenda kuwasihi
wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini kuendelea
kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza
majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo
mbalimbali inayotolewa na Serikali” alisema Biteko .
Kwa upande wake mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa manufaa ya soko jipya la madini
litasaidia kuziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini,
ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela
katika maeneo mengi ya nchi.
Aliongeza kuwa soko
hili litasaidia kuwezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa
kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la
kuuza na kununua madini.
aliendelea kufafanua
manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa
na kudhulumiwa na kuondoa vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa
vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya
wachimbaji wadogo.
Kwa upande wake
mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoani Arusha ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya
kudumu Bunge nishati na madini Catherine Magige alisema kuwa
Soko hili litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na
wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana.
Alitumia mda huo
kuwasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka
udanganyifu na matapeli tu
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiongea katika uzinduzi wa kituo cha uuzaji madini mkoa hapa |