Mkuu wa wa wilaya ya Monduli.Idd Hassan Kimanta akitoa shukrani mara baada ya kupokea vifaa tiba ikiwa ni kitanda cha upasuaji (OPERATING BED) chenye thamani ya milioni 19 kutoka katika shirika la Parthfinder
Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha
Shirika la
Parthfinder la kimataifa lililo sajiliwa hapa nchini Tanzania
linalofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Marekani
(USAID) limekabidhi vifaa tiba vyenye dhamani yilingi milioni 19,000,000 katika vituo vya afya vya wilayani Monduli.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja mradi wa shirika hilo Angelo Kihaga alisema kuwa shirika lao linatekeleza miradi mbalimbali kwa miaka mitano pia wanafanya kazi katika hifadhi za Taifa za (TARANGIRE NATIONAL PARK
ECOSYSTEM) na mradi wao unalengo la kusaidi sekta mbalilimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia watu,afya,mazingira,uzazi wa
mpango,cocoba na boma za mfano.
Alisema msaada huu ni moja lengo lililopo katika mradi wao wa miaka mitano ambao shirika linatekeleza ambapo alitaja baadhi ya vitu ambavyo wamevitoa kuwa ni kitanda kwa ajili ya mama kujifungulia,mikasi ,sindano ,glops pamoja na vifaa tiba vingine mbalimbali.
Kihanga alisema kuwa mradi wao wamelenga kufikia mikoa miwili ambayo ni mkoa mzima wa Arusha pamoja na Mkoa Wa Manyara pia watalenga zaidi kusaidia watu katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya pamoja na Mazingira
Akiongea mara baada yakupokea msaada huo mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta alishukuru shirika hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa shughuli za maendeleo wilayani Monduli na kuwahaidi kuwa atavisimamia vyema na kuvitunza ili kuweza kuendelea kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo hususa ni wamama wanaoenda kujifungua
Aidha mkuu huyo wa wilaya alilitaka shirika pamoja na mashirika mengine kuendela kutoa misaada mbalimbali hususa ni katika sekta ya afya kwa ajili ya vituo vya afya vya wilaya hiyo ya monduli.
Shirika hilo hilo la
Parthfinder la kimataifa lililo sajiliwa hapa nchini Tanzania
linalofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Marekani
(USAID)inatekeleza miradi mbalimbali kwa miaka mitano shirika hilo
linafanya kazi katika hifadhi za Taifa (TARANGIRE NATIONAL PARK
ECOSYSTEM) Kwa lengo la mradi wa watu,afya,mazingira,uzazi wa
mpango,cocoba na boma za mfano.