Na Woinde Shizza, Arusha
Wadau
wa Ujasiriamali mkoani Arusha wametakiwa kutoa ushirikiano sanjari na
kujitokeza katika mafunzo mbali mbali ya kada hiyo lengo likiwa kufikia
adhma ya serikali kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa mkurugenzi wa kampuni ya Zebra
Promotion Zuberi Mwinyi alisema kuwa kama wajasirimali hawatakuwa na
ushirikiano na kutoa nafasi kwa yale wanayojifunza kuwapa wenzao lengo
la serikali halitafikiwa.
Amesema
kuwa ili elimu ya ujasiriamali iwafikie watanzania kwenye maeneo mbali
mbali nchini inahitajika nguvu ya ziada ambayo kila mmoja ashiriki kwa
yale aliyonayo kuyatoa kwa lengo la kuboresha uzalishaji na kipato kwa
wajasiriamali.
Amesema
kuwa serikali imeandaa maeneo ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo na vya
kati kwa lengo la vijana wa kike na kiume sanjari na wenye ulemevu
kujitokeza kuanzisha viwanda na kuachana na dhana ya kuajiriwa ili
waweze kujiajiri kufikia uchumi wa kati wa viwanda na kuwataka
kuchangamkia fursa hiyo.
“Ndio
maana kampuni ya Zebra Promotion imekuja na mafunzo kwa kila kata
kwenye mkoa wetu lengo likiwa ni kuwafikia vijana na kina mama hususani
wauza mboga mboga na matunda kwa kuwapa elimu ya teknolojia ya
kubadilisha mifumo ya maisha yao kwa kuwapa elimu ya uzalisha,uchakataji
wa bidhaa na utunzaji wa fedha na mitaji” alisema Mwinyi.
Amesema
kuwa masomo wanayotarajia kuyafundisha yamelenga kuwainua wajasiriamali
wadogo kwenye kata zao na kuanzia tarehe 24 mwezi huu wataanza na Kata
ya Ngarenaro kwa awamu ya pili baada ya awali kuwa na semina kama hizo
katika kata mbali mbali za jiji la arusha ambazo zilileta tija na
kuonyesha mwanga kwa kuinua vipato vya kinamama na vijana kwenye kata
zao
Alisema
kuwa kampuni yao imeendelea kufundisha uchakataji wa bidhaa za
sabuni,shampoo,pinatbata mafuta mbali mbali.utengenezaji wa
maandazi,ubuyu na keki, mishumaa.ufugaji bora wa kuku wa mayai na nyama
na sungura,kilimo cha uyoga,sanjari kilimo cha mboga mboga kupitia
kilomo nyumba(GREEN HOUSE) .
Amesema
kuwa semina hizo za uzalishaji na kuwatafutia masoko na mitaji
zinalenga kuwabaidilishi maisha kupitia sekta mbalimbali hapa nchini kwa
kuwawezesha kuwapa elimu ya kukuza mitaji kwa kupitia vikundi vyao vya
vicoba ili kuweza kukopesheka katika taasisi za kifedha hapa nchini.
Amesema
kwa kushirikiana na Taasisi ya Kaizen kutoka nchini Japan na Sido
watatembelea wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vikubwa mkoani hapa
kutoa elimu na kuitangaza teknolojia ya Kaizen ili kuweka maboresho
kwenye viwanda vyao ikiwemo mipangilio ya viwandani itakayoleta tija
katika uzalishaji wao.